YALIYOJIRI MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO MISSENYI DEC 29,2016
KUPE ametajwa kuwa chanzo cha ufugaji na uzalishaji hafifu
wa maziwa kiasi kwamba hata bei ya maziwa kupaa mpaka kufikia shilingi 1200 kwa
lita wilayani Missenyi na wakati katika nchi jirani ya Uganda yakiuzwa kwa
shilingi 200 kwa lita.
Kauli hiyo ilitolewa na mbunge wa jimbo la Nkenge balozi Deodarus
Kamala wakati wa mkutano wa wa dau wa maendeleo ulikuwa ukifanya tathimini ya
maendeleo katika jimbo la Nkenge uliofanyika juzi katika halimashauli hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa sababu iliyosababisha wafugaji wa
Uganda kufanikiwa katika ufugaji na kuzalisha maziwa nipale tu walipo jikita
katika kutokomeza mdudu hatali kupe.
"Kwa hali ya kawaida wewe ni mfugaji lakini
hujatengenezea mazingira mzauri ya N'gombe hao unafikli utazalisha nini zaidi
ya kupata maziwa kidogo yasiyo toshereza na mwisho wasiku mifugo inakufa tu
hivyo kuna kila sababu ya wataaramu wa mifigo wilayani Missenyi kutoa elimu kwa
wafugaji na kuyafufuwa majosho ya kuoshea N'gombe ambayo sasa
yamepotea"alisema Kamala.
Kamala alisema kuwa Missenyi kuna kupe wa kutosha sasa
tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha tunawatokomeza kwa kutafuta dawa na kuwaosha
N'gombe wetu ili tuweze kuzalisha maziwa ya kutosha yatakayo tuwezesha kuwa na
viwanda vya maziwa.
Makula alisema kuwa hapo awali yalikuwepo majosho 20 ambapo mpaka kufikia sasa yapo majosho matatu tu ambayo yamebakia yakifanya kazi ila hayana ubora wowote kwasasa.
Alisema kuwa Majosho 17 ambayo hayafai kwa matumizi ya wakati huu yamezungukwa na makazi ya watu kiasi kwamba sio rahisi kukusanya N'gombe na kuwaosha katika majosho hayo.
"Majosho yakisha zungukwa na makazi ya watu yana poteza sifa ya kufanya kazi iliyolengwa lakini pia wafugaji wanatakiwa kujipanga angarau kufanya ufugaji uliobora"alisema Makula
Pia alisema kuwa wilaya hiyo inamachinjio ya hali ya kati hivyo kuna sababu ya kutengeneza machinjo yaliyo bora kibiashara
Mdau wa Maendeleo ya Jimbo la Nkenge Samuel Lugemalila akichangia kuhusu uwepo wa fursa katika ufugaji wa Samaki na Nyuki kwa kuzingatia mazingira ya Wilaya ya MissenyiMdau akitoa hoja katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Missenyi ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge
Naye afisa mifugo msitaafu wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Gilbert Makwabe alifafanua jinsi anavyo mjua kupe alivyo na athali kwa N'gombe .
Aidha alisema kuwa N'gombe anapo ingiliwa na kupe anadhofika, anapata ugonjwa wa Ndigana,Ndigana baridi,ugonjwa wa kukojoa damu, kupe anapunguza damu ,uzito unapungua, N'gombe anapata homa, anapoteza hamu ya kula, hivyo vifo vya mifugo kuongezeka kwa wingi pia husababisha mifugo kuwa na kizuguzungu, kutokana na hali hiyo pato la mfugaji lazima lipungue.
Pia dawa za kuoshea N'gombe zinauzwa kati ya elifu 40000 ambapo dawa inayoweza kutumika kwa lita elufu tano za maji zinatakiwa zitumike lita tatu ambao samani yake ni 120,000
Kwa upande wadawa za kuoshea mgongoni zinauzwa kati ya elfu 5000 , na elfu 3000 zote hizo zinatumika kwa kuondoa kupe.
Mwisho.
Hoja mbalibali kutoka kwa wadau walioweza kuhudhuria mkutano huo ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Kagera, Bi. Constancia Buhiye akitolea Jambo ufafanuzi
Muonekano wa Jengo la Halmashauri ya Missenyi kwa nyuma.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Dec 29,2016
Sehemu ya wanahabari mara baada ya Mkutano huo Dec 29,2016.