Pia shule hiyo haina nyumba hata moja ya Walimu licha ya kuwa na walimu 9 na iliyojengwa miaka 10 iliyopita imeishia renta huku serikali ya kijiji cha Kasindaga ikijenga ya miti ili walimu hao wapunguze kutembea umbali wa kilomita 18 kila siku kwenda kufundisha wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wakielekea katika Vyoo na walimu bado wanajisaidia katika mazingira hayo
Walimu wa shule hiyo na wanafunzi pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Kasindaga Mathias Bishobo wamethibitisha kuwepo wa changamoto hizo na kwamba wananchi wanajitahidi kuchangia vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao ili kuboresha Miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kuiomba serikali kuchangia vifaa vya ujenzi vitokavyo viwandani
#Bukobawadau Jan 29,2017.
0 comment:
Post a Comment