Bukobawadau

Hospitali ya mkoa wa kagera yapatiwa vitanda 20 na magodoro 20 kwaajiri ya wodi ya wajawazito na wazazi.


Na Mwandishi wetu
Bukoba.
 
AHADI ya vitanda 20 na magodolo 20 vyenye tahamani ya milioni 11 kwaajili ya wodi ya wajawazito na wazazi imetimizwa leo baada ya mkuu wa mkoa wa kagera Meja jenerali mstaafu Salim Kijuu kupokea vifaa hivyo mkoani hapo.
 
Ahadi hiyo ilitolewa mwaka jana na waziri wa afya jinsia wazee na watoto ummi Mwalimu alipokuja kwenye uzinduzi wa wodi ya wajawazito na wazazi ililoyojengwa na Japaigo mwaka 2016 tarehe 8.
 
Hata hivyo vifaa hivyo vimekabidhiwa na meneja wa (MSD) Muleba Egidius Rwezahura.
 
Naye mganga mfawizi wa hospitali ya mkoa wa Kagera Juma Nyakina alitoa shukrani kwa waziri wa afya kwa kutimiza ahadi yake.
 
Nyakina alisema kuwa wodi hiyo ilikuwa na vitanda 46 na baada ya upanuzi wodi hiyo inauwezo wa kubeba vitanda 66 hivyo hakuna mama atakeye lala chini.
“Kwa siku wodi ya wajawazito na wazazi ilikuwa inawapokea akina mama kati ya 15 hadi 25 hivyo kutokana na upanuzi wa jingo hilo na vifaa hivi akimama wafurahi sana”anasema Nyakina
 
Mwisho.
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau