Bukobawadau

UCHAGUZI WA MARUDIO, ACT WAZALENDO NA UMOJA WA WAPINZANI: HOJA ZA JULIUS MTATIRO NA PROF. KITILA MKUMBO

"Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive) kwani pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe kwenye kata chache (kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo ni alert call kwamba ACT is needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze ku BEHAVE like a true party wakati UKAWA pia ikiiandalia mazingira kisaikolojia"-Julius Mtatiro
..............................

"Shukrani kwa uchambuzi mzuri, as always. Hatua ya kwanza katika kushirikiana ni kuheshimiana na kukubali kwamba kutofautiana mawazo na mikakati ya kisiasa ni jambo jema badala ya kupeana majina. Binafsi nilishangaa sana kuona kuna kata kulikuwa na wagombea wa CDM na NCCR. Nilielewa kwa CUF kwa kuwa zipo mbili. Sasa kama UKAWA ni CUF, CDM, NCCR na NLD. Kisiasa NLD haipo, ipo kisheria tu. CUF ndio hiyo. Kwa hiyo politically speaking UKAWA ya sasa ni CDM na NCCR. Ukitaka kuwa serious zaidi utaona kwamba NCCR inapoelekea ni kubaki kuwa chama kilichosajiliwa tu kisichokuwepo katika ulingo wa kisiasa. Ni kwa sababu hii Ndugu Kafulila alihamia CDM. Vinginevyo Kafulila alikuwa hana haja ya kuhama. Kwa hiyo, technically and politically speaking, UKAWA ya sasa ni CDM.
Even more technically and politically speaking UKAWA ya sasa ni jina! Hapa ndipo pakuanzia. Tunahitaji kujiunda upya kama tunataka ushirika. Hatua ya kwanza kabisa katika kushirikiana ni kuheshimiana. Kubezana hakuwezi kuzaa ushirikiano na hii imetugharimu miongo yote tangu mfumo wa vyama vingi uanze. Kila mara chama chenye nguvu zaidi huvidharau vyama vingine na kuvipa majina mabaya. Mbaya. Tujisahihishe. Otherwise, tunakushukuru comrade Julius S. Mtatiro kwa kutambua kazi tunayofanya kisiasa. Tunaendelea. Sie uchaguzi huu umetupa nguvu zaidi kwenda kwa wananchi. Huko ndiko heshima ya kisiasa iliko. Tukitoka huko tutakutana mezani na kila chama kuweka hesabu zake"-Prof. Kitila Mkumbo
Next Post Previous Post
Bukobawadau