Bukobawadau

UTANDAWAZI UMETAJWA KUHARIBU MAADILI YA WATOTO WA KIKE

Na Mwandishi wetu.
Bukoba.

UKUWAJI wa sayansi na tekinolojia umetajwa kuwa chanzo cha watoto kukosa maadili kuanzia ngazi ya familia hadi jamii.

Kauli hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti wakati walipohojiwa na mwandishi wa Mtanzania.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini Mrushidi Ngeze ambae pia nidiwani wa kata ya Rukoma, Diwani wa kata ya muhutwe wiyani muleba Magongo Justus pamoja na Maria Ishengoma mkazi wa Kagondo manispaa ya Bukoba.
Mrushidi Ngeze alisema kuwa utandawazi umesababisha watoto wakike kupotea katika maadili ya kitanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo utandawazi ulipokuwa mdogo.


"Kwa miaka ya Nyuma watoto wakike walimariza darasa la saba wakiwa na utii pamoja na usikivu ambaopo binti alisomeka kama barua tofauti na sasa ambapo binti haoni shida kuvaa hata mavazi yasiyofaa"alisema Ngeze

Hata hivyo alisema kuwa jambo lingine ambalo limekuwa kikwazo kwa watoto wakike ni muingiliano katika jamii umeongezeka tofauti na miaka ya nyuma ambapo wanafunzi wa lisoma katika shule wakiwa ni wao tu hivyo ilikuwa ni lahisi hata mzazi kumzibiti mtoto wake kutokana na kutokuingiliana na watu wengine.

Lakini pia kwa upande mwingine serikali bado inalojukumu la kuweka mkazo kwa watoto wakike wawapo mashuleni nahata nyumbani kwani mtoto ni wawote sio wa mtu mmoja.


"Nitumie nafasi hii kuiomba serikali kuiweka sheria ya kuwazibiti watoto wakike hasa kwenye kumbi za starehe na hata kwenye sherehe za usiku kuwe na limiti kuwa mtoto mwenye umri frani hatoluhusiwa kuingia kwenye ukumbi wowote"alieleza mwenyekiti huyo
"Niwaombe viongozi wa dini kushikiana wote kuhubili maadili kwa wazazi na walezi na watoto pia ndipo tutawasaidia watoto wakike"alisisistiza

Naye Diwani Magongo Justus alisema kuwa kiwango cha watoto wanaozaziwa katika familia nao nichanzo cha watoto kupoteza maadili katika jamii.
"Mfano ' utamkuta mzazi anawatoto zaidi ya kumi japo watoto ni zawadi kutoka kwa mungu lakini uwezo wa mzazi ni watoto watatu lakini anakumi hivi unafikilia nini kitakachotokea kwa watoto hao"alisema Magongo


Aidha alisema kuwa utamkuta mzazi hajui watoto wamekulaje wamelalaje' na wakati mwingine watoto unawakuta wanajitegemea, hawapati haki ya malezi, pamoja na haki ya elimu, mzazi nabakia akisema kuwa bora nimezaa .


"Inafika wakati watoto wanaposikia sehemu kuna harusi au msiba wanakwenda wote kula huko bila ya mzazi hajui huko wamekula kwa kunyaghanyana au kwa kukimbizana kitu ambacho ni hatari mpaka inafika wakati mzazi anasema bora watoto wamekula huko nipumue kitu ambacho ni hatali sana katika jamii na katika marezi ya mtoto wa kike"alisema Magongo
Maria Ishengoma aliongeza kuwa jamii inatakiwa kuendeleza marezi ya wazazi wa zamani ambayo yaliwafanya watoto kuwa watii kwa kila mtu.
"Mimi nimezaliwa mwaka 1980 na ninawatoto watatu sasa wote ni wakike, wakati ninakuwa katika famila yetu kira siku tulielezwa kuwa kila mtu unaekutana naye njiani unapaswa kumuheshimu kama unavyo mtii mzazi wako ikiwa ni pamoja na kumkuta na mzigo ukamsaidia nahata ungeagiza usinge kunja shingo"alisema Ishengoma


Alisema kuwa kwasasa utii haupo tena hata kama mzazi atakuwa anajitahidi kiasi gani bado mtoto anakuwa mgumu kugeuka na kuwaheshimu wazazi na hata wasio walezi wao.
Nitoe wito kwa wazazi na walezi wote kushikamana katika kufunza watoto wakike mambo mema hasa kuvaa vizuri na kuwa watii pamoja na kujituma katika masomo.
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau