Bukobawadau

WATUMISHI WATATU WA MANISPAA YA BUKOBA WASIMAMISHWA KAZI

SIKU moja Baada ya Rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania kumaliza ziara yake mkoani Kagera watumishi watatu wa manispaa ya Bukoba wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa madai kuwa thamani ya fedha zilizotumika haziendani na na muonekano wa majengo yaliyokarabatiwa katika shule ya sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM mkoani humo.
Hatua hiyo imefutia agizo la rais Dr John Pombe Magufuli baada ya kukagua ukarabati wa majengo hayo ambayo yalitumika kuwahamishia wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule ya sekondari Ihungo na Nyakato kutokana na tetemeko la ardhi na kubaini kuwa yapo chini ya kiwango cha fedha kilichotumika ni tofauti na uhalisia katika ukarabati huo.
Katibu tawala mkoa kagera Diwani Athumani aliwasimamisha watumishi hao akiwemo mhandisi aliyesimamia ukarabati huo Andondile Mwakitaru ,pamoja na mafundi sanifu Constatine Felex na Charles Kafumu baada ya kufanya ukaguzi na kubaini kuwa mradi huo ulijengwa chini ya kiwango
Awali akihojia na katibu tawala Diwani Athumani ,mhandisi Andondile Mwakitaru amesema ukarabati huo umegharimu shilingi milioni 19 huku fedha ambazo zilitengwa ni milioni 23.
Hata hivyo Athumani amemwagiza kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Chibhunu Rukiko kuteua wasimamizi wengine katika mradi huo wakati watuhumiwa wakisubiri kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
“Kutokana na changamoto hii kila moja anaweza kuona kwa macho yake kinachoendelea hapa sasa ili kila mtu asiwe na tafisri yake hivyo tupishe uchunguzi ufanyike na pale itakapo onekana nini kimefanyika basi ukweli utawekwa wazi kama nilivyofanya zoezi hili kwa uwazi na hakuna atake onewa hapa hivyo tusubili”alisema Athumani.
Aidha” Nakuagiza kaimu mkurugenzi hakikisha mnafanyamakabiziano katika vifaa vyote hata msumari ukabidhiwe na kesho saa moja asubuhi kabla sijaingia katika majukumu mengine uje na timu nyingine itakayo endelea na ukarabati katika shule hii”alisema katibu tawara huyo
Alitoa wito kwa wakurugenzi wote mkoani kagera kujenga tabia ya kuwa wafatiliaji miradi ya maendeleo ya jamii iyakuwa ikiendelea maeneo yao vinginevyo kila siku changamoto kama hizi zitakuwa zinajirudia katika halmashauri mnazozisimamia.
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau