WEMA SEPETU AONGEA NA WANAHABARI ATANGAZA KUAMIA CHADEMA
"Kama nimechukua hata shilingi elfu kumi toka chadema, naomba kaburi la baba yangu lititie kule Zanzibar" -Wema Sepetu
"Nimeonewa na nimefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama. Mapenzi ni nipe nikupe, yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi"-Wema Sepetu
"Nimekuwa nikipewa ushauri & kuonywa kuwa nitafanywa vibaya, nisifanye hivi. Nimeshavaa magwanda sasa, nipo tayari kupigana"-Wema Sepetu
"Natamka rasmi nimeamua mwenyewe kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda CHADEMA"- Wema Sepetu
"Ni kweli mimi na Wasanii wenzangu tunaidai pesa nyingi CCM. Tukifuatilia tunaambiwa tukamdai Kikwete."- Wema Sepetu