Bukobawadau

MATUKIO YA PICHA SHUGHULI YA MATANGA YA BALOZI RWEGASIRA NA ESTHER RWEGASIRA



Familia ya Marehemu Balozi Joseph Rwegasira na Mama Esther Rwegasira,siku ya Jana Feb 28,2017 wameungana na ndugu jamaa na marafiki katika shughuli ya Ibada ya kumbukumbu na kuanua matanga iliyofanyika nyumbani kwao Kijijini Bukombe Kanyigo na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

Wanafamilia wakiweka Maua na Mashumaa kwenye kaburi la mpendwa wao Mama Esther Rwegasira shughuli iliyofanyika Jana Jumanne Feb 28,2017.
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea kwa wanafamilia.
Marehemu Mama Esther Rwegasira enzi za Uhai wake pichani
Simanzi kubwa kwa Bi Joanitha Rwegasira kama anavyo onekana mara baada ya kuweka mashada ya maua.
 Mr Shuli wakati akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Mama mkwe wake.
 Tuendelee kuwaombea wazazi wetu wapumzike kwa AMANI
 Shada la kwanza kabisa kwenye kaburi la Marehemu Esther Rwegasira

Mapadre wakiendelea kuongoza Ibada maalum ya kumbukumbu iliyoandaliwa na familia ya Marehemu Balozi Joseph Rwegasira

Shughuli ya Ibada ikiendelea kushoto Bwana Tibaijuka (Julius) akiwa na baba zake wadogo.

Ibada hiyo imeongoza na Fr.Medericus akishirikiana na paroko wengine.

Waumini wakiendelea kushiriki Misa maalum ya kuwaombea marehemu wapendwa wetu tunawaombea Mwenyenzi MUNGU mwingi wa Rehema ampe pumziko la milele

Picha ya Marehemu Balozi Joseph Rwegaziga na Mke wake Esther Rwegasira wakati Ibada inaendelea.
Wanakwaya wakiwajibika kwa nyimbo za kumsifu Bwana
Sehemu ya wanafamilia



Joanitha na Mme wake Shuli wakati wakiendelea na Misa ya kuwakumbuka wapendwa wazazi wao

Sehemu ya Mapadre wakati tukio la Waumini kutoa sadaka likiendelea


Waumini wakiendelea na Ibada ya kumbukumbu ya Balozi Rwegasiri na Mama Esther Rwegasira

Waumini wa Kikatoliki wakiendelea na Ibada hiyo iliyofanyika jana Jumanne Feb 28,2017

Pichani anaonekana Bi Rukia Goronga na Kaka yake Rasheed Goronga.

Muendelezo wa matukio wa picha kutoka eneo la Ibada Nyumbani kwa Marehemu Balozi Rwegasira


Bwana Shumbu na Bwana Kipara wa Stendi ya Soko kuu Bukoba wakiwa wameungana na familia hiyo kijijini Kanyigo Wilayani Missenyi
Mr. Rahym Kabyemela ameweza kushiriki shughuli hiyo
Wadau wakipata picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.

Mtu na Shost wake pichani ni Bi Julieth na Bi Asimwe Jovitha Njunwa.

Matukio yote ni kwa hisani ya Bukobawadau Media.

Msemaji wa familia akitoa neno la shukrani.

Katika picha ya pamoja na Bwana Julius ( Tibaijuka) Rwegasira aliyeteuliwa kama msimamizi wa familia hiyo.

Kiongozi wa Ukoo (Omgurusi) wakati akimsimika Bwana Julius (Tibaijuka) Rwegasira kwa kumkabidhi zana za kimira kama kiongozi wa familia ya Marehemu Balozi Joseph Rwegasira katika shuhhuli iliyofanyika siku ya Jana Jumanne Feb 28,2017 Nyumbani kwao kijijini Bugombe Kanyigo Wilayani Missenyi.

Bro Rasheed Goronga pichani kushoto.
Dr.Mboneko akimpongeza Kijana Julius (Tibaijuka) Rwegasira mara baada ya kusimikwa rasmi kama msimamizi wa familia.

Pongezi za hapa na pale zikiendelea kwa Bwana Rutta Julius Rwegasira mara baada ya tukio la kusimika kama msimamizi wa familia, tukio lililofanyika siku ya jana nyumbani kwao kijijini Kanyigo

Salaam na mkono wa pngezi kwa Bwana Tibaijuka
Furaha na pongezi vikiendelea .

Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika Shughuli ya matanga ,mwaka mmoja baada ya kifo cha Marehemu Balozi Rwegasira na takribani Mwaka mmoja kifo cha Mke wake Marehemu Esther Rwegasira
Katika picha ya pamoja Bi Joanitha Rwegasira na Kaka yake Julius (Tibaijuka )Rwegasira

Bro Kazimoto pichani kulia akifurahia jambo


Taswira mbalimbali muda mchache baada ya kuteuliwa kwa Msimamizi wa familia

Kinachoendelea ni watu wote kupata huduma kabambe ya Chakula kilichoandaliwa na 'Mama Mussa' pichani kushoto
Wageni waalikwa wakipata huduma ya Chakula.

Huduma ya Msosi ikiendelea..


Taswira mbalimbali huduma ya Msosi safi ikiendelea...

Menu safi iliyoambatana na kitoweo cha 'Senene'



Wadau pichani ni Rama, Rasheed na Jamal Issa marafiki wa familia.



Baadhi ya wanafamilia kama wanavyo onekana kupitia picha

Mdau Rutta mmoja kati ya Watoto wa Marehemu Balozi Joseph Rwegasira aliyewahi kuwa Waziri wa Zamani wa Ushirikiano wa  kimataifa.


ENDELEA kuwa nasi kwa matukio zaidi ya picha.......

Sasa unaweza kupata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD
Next Post Previous Post
Bukobawadau