Bukobawadau

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU AKABIDHIWA OFISI RASMI LEO MJINI DODOMA


Katibu mkuu wa wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwikapo na Naibu katibu mkuu Dkt.Ave Maria Semakafu leo wamepokelewa na kukabidhiwa ofisi zao katika makao makuu ya ofisi za wizara hiyo zilizopo Katika chuo kikuu cha Dodoma – UDOM, mkoani Dodoma.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo Dkt.Akwilapo ameahidi kuendeleza ushirikiano, kufanya kazi kwa bidii mambo ambayo yalikuwepo wakati wa uongozi wa Katibu mkuu Maimuna Tarishi ambaye hivi sasa amehamishiwa katika ofisi ya waziri mkuu.
 Pichani Naibu Katibu mkuu Dkt.Ave Maria semakafu akisalimiana na watumishi wa wizara ya Elimu hii leo Mara baada ya kupokelewa katika makao makuu ya ofisi za wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia zilizopo mkoani Dodoma.
 Dkt.Ave Maria semakafu akiwa anapokea Ua linaloashiria kukaribishwa Wizara ya elimu.
 Dkt.Leonard Akwilapo akiwapunfia mkono watumishi waliojipanga kwa ajili ya kumpokea na kumkaribisha Wizarani, Dodoma. 
 Sky Akwilapo akipokea Ua kama ishara ya kukaribishwa katika Ofisi za Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia zilizopo Mkoani Dodoma.
 
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau