Bukobawadau

MAELFU WAMZIKA MAREHEMU DOMINICK RWEHUMBIZA MUGOMBA KIJIJINI KANYIGOShughuli ya Mazishi ya marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba (81),imefanyika siku ya jana Alhamis 30,2017 Nyumbani kwake Kijijini Kanyigo Wilayani Missenyi,Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Vyama na Serikali.

Mapadre wakiongoza msafara wa kutoa ndani Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba
ENDELEA KUWA NASI MPAKA MWISHO KWA MTIRIRIKO MZIMA WA MATUKIO..
Msafara wa kutoa mwili ndani kwa ajili ya kuanza kwa shughuli ya Ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Kanyigo -Nshumba Wilayani Missenyi alhamisi Marchi 30,2017

Endelea kuwa nasi kwa mtiririko wa matukio haya,kumbuka Matukio zaidi ya picha 200 yatapatikana katika ukurasa wetu wa facebook @bukobawadau media

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu mpendwa wetu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba aliyewahi kuwa katibu wa wilaya wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mjini Mwanza, Sengerema, Biharamulo na Bukoba Mjini mpaka kustaafu kwake.


Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na Sukari tangu mwaka 2010.

Mmoja kati ya watoto wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Dominick Mugomba pichani anaonekana Bi Domina Mutta katika hali ya Simanzi

Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza mnano tarehe 23/3/3017 alilazwa katika hospitali ya Mugana Wilayani Missenyi na baada ya kupimwa aligundulika ana ugonjwa wa figo,ndipo alipoamishiwa katika hospitali ya rufaa Buganda jijini Mwanza kwa matibabu zaidi ambapo alifikishwa tarehe 26/3/2017 saa moja na nusu usiku na kuaga dunia tarehe 27/3/2017 saa saba Usiku

Waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushiriki maziko hayo

Baadhi ya Wajuu wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Ibada ya kumuaga mpendwa wetu mzee Mzee Dominick Rwehumbiza ikiwa inaendelea
Ibada ya mazishi kumuaga mpendwa wetu Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza ikiwa inaendelea.


Haya ndiyo yaliyojiri katika shughuli ya maziko hayo ya Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Missenyi (zamani bukoba Vijijini)

Kushoto ni Mzee Kagashe ambaye ni rafiki mkubwa wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Msiba huu umewagusa watu wengi wakazi na wenyeji wa Kanyigo na vitongoji vyake


Mamia ya waombolezi wakiwa migombani yote ni katika kumuaga Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Taswira mbalimbali eneo la tukio Ibada ya mazishi ikiwa inaendelea

Umati wa waombolezaji waliohudhuria shughuli ya mazishi ya Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza siku ya jana alhamis machi 30,2017

Katikati anaonekana Mrs Philbart Nyerere.

Wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho zikiendelea

Mzee Haji Abbas na Mzee Pius Ngeze pichani

Umati mkubwa wa waombolezaji wakiwa na simanzi kubwa

Mamia ya waombolezaji wakishiriki Ibada ya mazishi.

Sehemu ya wanakwaya wakati Shughuli ya Ibada ikiwa inaendelea


Mwanzo wa kutoa heshima za mwisho

Baadhi ya waombolezaji wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea.

Mwili wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza ukitolewa heshima za mwisho..!

Mtendaji wa kata ya Gera akitoa heshima za mwisho kumuaga mpendwa Mzee Domenick Mugomba

Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea..Katikati ni Bi Domina Mutta ambaye ni binti wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Dominick Mugomba

Vilio vikitawala kwa wanafamilia wakati wa zoezi la kutoa heshima zao za mwisho


Bi Jeniveva akitoa heshima zake za mwisho.

Bwana Kamuzora,Mwenezi wa CCM Wilayani Missenyi akitoa heshima za mwisho.

Wanaonekana watoto wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Dominick Mugomba wakitoa heshima za mwisho.

Hakika ni simanzi na vilio kwa wanafamilia kumpoteza mpendwa wao
Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba ameacha watoto 12 wa kiume 6 na wa kike 6,Wajukuu 21 na Kitukuu 1.


Diwani wa kata ya Kanyigo akitoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba


Wawakilishi wa Umoja wa wanakanyigo waishio Dar es Salaam maarufu kama (TWEKA) twemanye kanyigo wakitoa salaam za rambirambi
Kutoka Jijini Dar es Salaam tunapokea salaam za rambirambi kutoka wanachama wa (TWEKA)


Msemaji wa Imarika Saccos Kanyigo akitoa salaam za rambirambi

Mzee Pius Ngeze akitoa salaam za rambirambi , yeye alibahatika kufanya kazi na Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza toka miaka ya 70

Wadau mbalimbali wakiendelea kuwafariji wafiwa


Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza likielekea eneo la makaburi

Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza likiingizwa kaburini


Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu likiingizwa kaburibu

Mubashara kabisa mamia ya waombolezaji wakifatilia kila kinachojiri eneo la kaburi.

Tayari Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza lipo ndani ya kaburi.
Fr. akinyunyuzia maji ya baraka kwenye kaburi.

Fr. akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Waombolezaji na wanafamilia wakisindikiza mwili wa mpendwa wao Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Wanafamilia wakiweka Udongo kwenye kaburi la mpendwa wao Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza,shughuli iliyofanyika jana alhamis achi 30,2017.

Bi Joanitha akishiriki kuweka udongo kwenye kaburiWatoto wa marehemu wakiweka Udongo kwenye kaburi la Mpendwa wao Marehemu Mzee Dominick Mugomba.

Zoezi la kuweka Udongo kwenye kaburi linaendelea.

Taswira mbalimbali eneo la kaburi shughuli ya maziko ya Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza kijijini Kanyigo Wilayani Missenyi.Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli ya maziko hayo yaliyofanyika siku ya jana Alhamis machi 30,2017.

Eneo la makaburi shughuli ya maziko ikiendelea

Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya mzee wetu Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza ambaye mpaka mauti yanmkuta alikuwa ni mshauri wa masuali mbalimbali ya Chama
Kwa pamoja watoto wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza wakiwa tayari kuweka shada la maua

Watoto 12 wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza wakiwa tayari kuweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa baba yao

Watoto wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza wakiweka shada la maua

Wajukuu wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza wakiweka shada lao la maua

Wanafamilia wakiweka mashada ya maua

Fr akiweka shada la maua


Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza hakuacha mjane, tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi AMEEN
Wadau wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza

Mama Prof .Baregu akiweka shada la maua.
Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza hakuacha mjane, tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi AMEEN
Bi Joanitha Rwegasira , rafiki wa familia hii akishiriki shughuli ya maziko iliyofanyika Kijijini Kanyigo siku ya jana
Mr.Daniel Mutta Mmoja wa wakwe wa familia hii akiwa tayari kuweka shada la maua.

Wakwe wa familia ya Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza wakiweka shada la maua kutoka kushoto ni Daniel Mutta na Prospa Palagha.

Muonekano wa nyumba ya Milele ya Marehemu Mzee wetu Dominick Mugomba

Mtu na Swahiba yake pichani ni Bi Domina na Bi Jeniveva mara baada ya shughuli ya mazishi


Watoto 6 wa kiume wa kuzaliwa na Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza
Baadhi ya Wajuu wa Marehemu Mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu

Baadhi ya wajukuu wakipata picha kwa ajili ya kumbukumbu.

Mzee Yassin wa Kanyigo pichani.

Kutoka ukweni pichani ni wazazi na wanafamilia ya Mr. Daniel Mutta ,hayupo pichani

Watoto wa kiume wa marehemu katika picha ya pamoja.

Muendelezo wa matukio ya picha baadhi ya wajuu wawakiwa na rafiki yao (pichani kulia) aliyefika kuwafariji


Taswira mbalimbali camera yetu ikiwa bado eneo la tukio

Wadau na wanafamilia wakichukua picha ya kaburi kwa ajili ya kumbukumbu

Taswira eneo la tukio.
Watoto wa marehemu katika picha kwenye kaburi la mpendwa Baba yao,apumzike kwa AMANI mzee Dominick Rwehumbiza Mugomba
BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIWE..!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau