Bukobawadau

RAIS MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA KATOLIKI LA KRISTO MFALME PAMOJA NA KANISA LA KILUTHERI KKKT MOSHI MJINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo akimsomea mstari wa Biblia kutoka kitabu cha Yeremia 17: 7-8 kabla ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo  akimkabidhi zawadi ya Msalaba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumuombea yeye pamoja na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiubusu msalaba huo aliopewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba nyimbo pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo  kabla ya kufungwa kwa ibada katika sehemu ya nje ya Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu Mstaafu Erasto Kweka mara baada ya Ibada katika Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo, Askofu Mstaafu Erasto Kweka, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadik, Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Ajira,na wenye wenye
ulemavu Jenista Mhagama  mara baada ya Ibada katika Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya Ibada katika kanisa la KKKT mjini Moshi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mstaafu Erasto Kweka mara baada ya kumalizika kwa Ibada katika kanisa la KKKT mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya Ibada katika kanisa la KKKT mjini Moshi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba nyimbo pamoja na waumini wengine katika ibada ya jumapili katika Kanisa la KKKT mjini Moshi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani katika ibada ya jumapili kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya jumapili katika Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme.
Baba Askofu wa Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani akimuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini pamoja na viongozi wa Kanisa la   Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme. PICHA NA IKULU

Next Post Previous Post
Bukobawadau