Bukobawadau

TIMU YA KAGERA SUGAR ''WANANKURUKUMBI'' WAIADHIBU SIMBA 2-1 UWANJANI KAITABA LEO

Timu ya Kagera Sugar maarufu kama Super Nkurukumbi leo wameza kuwafurahisha  Maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mpambano wao dhidi ya timu ya Simba katika mchezo wa ligi ya Vodacom.
 Hali ilionekana kuwa tete kwa wanamsimbazi mwanzoni kabisa mwa kipindi cha kwanza
Kocha Joseph Omog bado anahitaji miujiza ya kuondoa ukame wa mataji kwenye klabu ya Simba baada ya leo kupoteza mchezo muhimu mbele ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi ya Vodacom uliopigwa uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba. 
 Washambuliaji waliowahi kuichezea Simba Mbaraka Yusuph na Edward Christopher ndio walioiangamiza Simba na kuyeyusha ndotio za ubingwa msimu huu baada ya kufunga bao katika kila kipindi. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kubaki kileleni kwa kuwa na pointi 56 na Simba kubaki nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 55, huku timu hizo zikifanana kwa idadi ya michezo ya kucheza. Simba waliokuwa kileleni kwa muda mrefu msimu huu, waliingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi lakini kibao kiliwageukia na kujikuta wakilala kwa mabao 2-1.
 Mshambuliaji chipukizi Mbaraka Yusuph alianza kuifungia Kagera Sugar bao la kuongoza dakika ya 27, baada ya kufumua shuti kali lililomshinda kipa Daniel Agyei na kuiweka Simba kwenye presha kubwa ya kutafuta bao la kusawazisha. Mchezo huo uliendelea kwa Simba kucharuka na kufanya mashambulizi mengi lakini kipa wao wa zamani Juma Kaseja alikuwa kikwazo baada ya kudaka kila shuti lililopigwa kwenye lango lake. Mshambuliaji Ibrahim Ajibu mara kadhaa alijaribu kutengenezaa mipira ya hatari kwa Laudit Mavugo lakini walinzi wa Kagera Sugar walikuwa makini na kuondosha hatari zote langoni mwao na kufanya hadi mapumziko vijana wa kocha Mecky Maxime wakiwa mbele kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili wenyeji Kagera walikianza kwa kasi na iliwachukua dakika tatu kufunga bao la pili lililifungwa na Edward Christopher baada ya beki Juuko Murshid kushindwa kuzuia pasi ya Mbaraka Yusuph. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Simba na kuongeza kasi ya mchezo kwa kulisakama lango la Kagera Sugar lakini walishindwa kuipenya ngome ya timu hiyo iliyokuwa chini ya viungo Anthon Matogole na George Kavila. 
 Baada ya kuona mambo magumu kocha Joseph Omog aliamua kumpumzisha Ajibu na kumuingiza Mohamed Ibrahim ambae naye alizidisha kasi ya mashambulizi lakini bado mambo yalikuwa magumu kwao. Omog alilazimika kubadilisha mfumo wa uchezaji ili kupata ushindi na kumuingiza mshambuliaji Juma Luizio na aliyechukua nafasi ya Shiza Kichuya, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu licha ya kosakosa nyingi kwa kila upande. Jitihada za washambuliaji wa Simba zilizaa matunda baada ya dakika ya 61 kufanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Mzamiru Yasini, aliyeumalizia mpira uliotemwa na kipa Juma Kaseja kufuatia shuti kali la Juma Luizio.
 Bao hilo lilionekana kuwapa nguvu Simba na kuendelea kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Kagera lakini walishindwa kuzitumia vizuri nafasi walizozipata. Kocha Maxime naye baada ya kuona mambo magumu alimtoa mfungaji wa bao la pili Christopher na kumuingiza Themi Felix ambaye naye alionekana kuwasumbua sana mabeki wa Simba wakiwemo Murshid na Abdi Banda hata kuonyeshwa kadi za njano kufuatia kumchezea rafu Mbaraka Yusuph. Kipa Kaseja naye alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86 baada ya kupoteza muda kufuatia kasi ya Simba na mashambulizi mengi kuelekezwa kwenye lango lake. 
Hadi dakika 90 za mpambano huo zinakamilika Kagera Sugar waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuchupa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wakifikisha pointi 45 na kuishuhsa Azam kwenye nafasi nne wakibakiwa na pointi zao 42.
 Baadhi ya wadau wa Soka wakifuatilia mtanange huu
 Matangazo yakirushwa live kupitia Azam Tv. pichani ni Mdau wetu Steven akiwajibika...
 Wadau wasoka wakifuatilia  mpambano huo ulioweza kukusanya maelfu ya watazamaji kutoka maeneo mbalimbali mkoani Kagera
 Zacharia Hans Poppe akiwa hana hamu baada ya kushuhudia Timu ya Simba ikinyukwa bao 2-1 na Timu ya Wanankurukumbi Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kagera Sugar leo hii jumapili.

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime akisalimiana na Mayanja wa Simba leo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.
Mashabiki waliingia kwa wingi kwenye Mtanange huo ulikuwa na hamsha hamsha ya kila aina yake.

Kikosi cha Simba kilichoanza
Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wakiwa jukwaa kuu kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar kuanza.

Kikosi cha Kagera Sugar kikiomba kabla ya mtanange kuanza
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi Simba ya Jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusuph

Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haamini kilichotokea baada ya timu yake kufungwa bao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa uwnaja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mbaraka akipongezwa kwa bao
Anaonekana katika sintofahamu Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog 
 Ndivyo unavyosomeka ubao wa matangazo  mpaka tunaelekea mapumziko

Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haaminiTimu yake ikiwa nyuma ya bao 2-0
Hadi mapumziko Simba walikuwa nyuma ya bao 1-0
Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .

Mshambuliaji wa timu ya Simba Kichuya akichanja mbuga
 Mlinda mlango wa Kagera Sugar Juma Kaseja akianzisha mashambulizi
Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea
Kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla akiachia Shuti kali ambalo lilipanguliwa na Kipa Juma Kaseja
Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana  ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Muonekano wa Jukwaa kuu Uwanjani kaitaba leo April 2,2017
Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar akiwa amebebwa na Wachezaji wa Kagera mara baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.

Simba walipata bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 61 na mtanange kuwa 2-1Naaam...! wanaonekana sehemu ya Mashabiki wa tiimu ya Kagera Sugar wakiwa pamoja na Mlinda mlango wao Juma Kaseja.
Mtanange ulipomalizika Kipa Kaseja alipewa zawadi na Mashabiki wa Kagera Sugar pamoja na Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 Mubashara kutoka Uwanjani Kaitaba ,mwanalibeneke Mc Baraka katika interview na Mdau Jamal Kalumuna Jamco
 Panapo Jengo la CCM jirani na Uwanja wa Kaitaba, wadau wakifatilia soka free .Photo Credit;faustine Luta.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa uwanzani Kaitaba mpaka dakika 90 za mpambano huo zinakamilika Kagera Sugar waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuchupa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wakifikisha pointi 45 na kuishuhsa Azam kwenye nafasi nne wakibakiwa na pointi zao 42.
#bukobawadaumedia
Next Post Previous Post
Bukobawadau