Bukobawadau

MURSHIDI NGEZE AAHIDI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA TARAFA RUBALE.

Pichani Mh. Murshidi Ngeze akisisitiza jambo wakati akiongea na Wananchi wa tarafa Rubale katika Mkutano wa Maendeleo Juni 3, 2017.

Na Dulla, Kasibante Fm.

Diwani wa Rukoma na Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze, ameaahidi kutoa vifaa vya michezo kwa Timu ya Tarafa Rubale, ikiwa ni pamoja na Mipira na Jezi.

Ahadi hiyo imekuja mara ya baada ya kufikishiwa kilio cha Timu hiyo ya Rubale Fc, Na mwakilishi wa timu hiyo Ndg, Abdullatif Yunus (Dulla), katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Katani Rubale.

Akiwasilisha ombi hilo Dulla, amemuomba Mwenyekiti  huyo kuwa Timu ya Rubale Fc, ni Timu yenye kujitahidi katika maendeleo ya Soka ndani  na nje ya Tarafa Rubale, ikiwa ni pamoja nakucheza mechi mbalimbali za kirafiki na kushinda, lakini changamoto kubwa imekuwa ni kuazima jezi kila inapofika wakati wa kucheza mechi hizo, hivyo kumuomba Mh. Ngeze kuisaidia jezi katika kuinua na kuendeleza soka lao.
Mh. Ngeze kama mdau wa michezo na burudani,  nae bila hiyana akalipokea ombi hilo na kudai kulifanyia kazi ndani ya kipindi kifupi kijacho. Ikumbukwe kuwa Mwenyekiti huyo wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba ndiye Mdau Pekee ambae ameweka rekodi  ya kumleta msanii mkubwa Diamond Platnum, kwa mara ya Kwanza katika Wilaya za Bukoba, Bukoba Vijijini, Muleba  na Karagwe
Photo Credit: Allawi Kaboyo

Next Post Previous Post
Bukobawadau