Bukobawadau

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 47 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 14 JUNI 201

#Katika nchi yetu wanawake na wanaume wana haki sawa ya kupata na kutumia Ardhi.
#Sheria ya Ardhi inaelekeza kuwa haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kufanya miamala inayohusiana na ardhi itakuwa sawa na haki ya mwanaume kwa viwango na masharti yale yale.
#Serikali imeondoa jumla ya tozo 80 na kupunguza viwango tozo 4 katika tasnia ya mazao pekee kati ya jumla ya tozo 139 zilizopo.
#Serikali ipo tayari kuondoa kodi na tozo mbalimbali za mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi zisizokuwa na tija kama ilivyofanya mwaka 2016/2017.
#Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha maeneo yote ya umma yanapimwa na kupatiwa hati miliki yakiwemo shule,vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa matumizi mbalimbali ya umma.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*
Next Post Previous Post
Bukobawadau