Na: Sylvester Raphael
Hatimaye mkutano wa ujirani mwema kati ya
Tanzania na Uganda umemalizika leo Julai 29, 2017 majira ya jioni kwa
Mawaziri wa nchi hizo mbili kutiliana saini hati za makubaliano ya
utekelezaji wa masuala makuu manne ya ushirikiano katika maendeleo
waliyokubaliana kwenye mkutano huo wa siku moja.
Akitoa Taarifa mara baada ya makubaliano na kutiliana saini katika hati
za makubaliano Waziri wa Mambo ya nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa alisema
yeye akiongoza jopo la Mawaziri kumi kutoka Uganda pamoja na wataalam
wengine wamefurahishwa sana na Mkutano huo kwani umekuwa wa mafanikio
kwao.
Aidha Mhe. Kutesa alisema kuwa katika Mkutano huo wamekubaliana
masuala makuu manne ambayo yanahusu Kuhakiki mipaka ya kati ya nchi
mbili, pili Huduma za maji kutoka Mto Kagera, Tatu Biashara baina ya
nchi mbili na nne Kuhusu suala la nishati ya Umeme.
Akitoa
ufafanuzi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dk.Augustine Mahiga alisema kuwa kuhusu Suala la Mipaka wamekubaliana
kuongeza alama za mipaka ili mpaka uonekane vyema kati ya nchi mbili ili
kuondoa migongano inyoweza kujitokeza maeneo ya mpakani kwasababu
mipaka hiyo iliwekwa na Wakoloni miaka mingi iliyopita.
Pili Dkt.
Mahiga lifafanua suala la Huduma ya maji katika Mto Kagera na kusema
kuwa nchi ya Uganda wanayo matatizo ya maji kwa baadhi ya sehemu mpakani
na Tanzania na maji yanapatika Mto Kagera kwa upande wa Tanzania kwa
hiyo katika suala hilo Waganda wameomba na kukubaliana na Tanzania
kujenga mabwawa na malambo kwaajili ya kunywesha mifugo yao.
“Suala hilo tumekubaliana lakini taratibu zote za mazingira
zitafuatwa ili kusijekukatokea uharibifu wa mazingira na uvujanjaji wa
sheria za mazingiara.” Alisistiza Waziri Dkt. Maiga. Kuhusu suala la
Biashara Dkt. Maiga alifafanua kuwa wamekualiana kuimarisha biashara
kati ya nchi mbili pamoja na kuwa nchi hizo zote zipo katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kuhusu Nishati ya Umeme Waziri Dkt. Maiga
alisema kuwa mji wa Bukoba unapata umeme kutoka Uganda kwa hiyo Tanzania
imekuwa ikipata nishati hiyo toka Uganda lakini kwa sasa Tanzania pia
inatarajia kuzalisha umeme wa kutosha ambapo wamekubaliana pia kuwa mara
ya umeme huo kuwa umepatikana Tanzania pia itawauzia Umeme Uganda.
Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya ELCT Bukoba ulihudhuliwa na
Mawaziri kutoka Tanzania saba pamoja na wataalam mbalimbali wakiongozwa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dk.Augustine Mahiga. Aidha, kwa upande wa nchi ya Uganda uliongozwa na
Waziri wa Mambo ya nje Mhe. Sam Kutesa pamoja na Mawaziri kumi
wakiambatana na Wataalamu mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment