Bukobawadau

SIMULIZI FUPI ZA KUSISIMUA

Nilirudi nyumbani nakukuta nyumba imefungwa, nilishangaa kwani nilijua mwanangu atakua shule na Dada wa kazi atakuepo. Lakini sikumkuta, niligonga sana mlango kwani funguo nilikua nimesahau ofisini. Baada ya kuona kimya niliamua kumpigia simu mume wangu na kumuuliza kama amekaribia kuja aliniambia yuko njiani hivyo nilikaa kumsubiri.

Dakika tano baadaye mume wangu alikuja na ikaanza kazi ya kumtafuta mtoto, sijui kwanini lakini nilihisi kitu kibaya. Lakini muda haukupita binti yetu wa kazi alikuja na nilipomuuliza alipo mtoto alisema hajui ila kabla hatujatulia mtoto wetu alikuja. Alikua kachoka na anatembea kama mlevi vile, alisalimia na nilimuuliza katoka wapi hakusema chochote alibaki kimya.

Nilirudi ndani lakini sikujisikia sawa, nilijua lazima kuna kitu. Nilianza na Dada wakazi kumuuliza lakini hakujibu, milikua mkali kuuliza ni kitu gani alikaua nafanya lakini bado hakujibu chochote. Baada ya kumaliza naye nilirudi kwa mtoto, sikutaka kuongea naye kwa ukali nilianza kumuuliza alikua anafanya nini lakini hakujibu.

Baada ya kuona vile niliamua kuwa mkali, nikimtishia kusema kwa Baba yake, aliniambia basi ataongea, ndipo aliniambia alikua anafanya mapenzi na Dada. Nilishangaa lakini alianza kunisimulia kila kitu, kwamba kila siku akitoka shule wanaenda kwenye nyumba moja mbovu hapo jirani na kufanya mapenzi.

Wakati mwingine hubaki chumbani kwa dada ambapo walikua wanafanya mambo yote. Alinielezea mambo mengi ambayo kweli yalinichanganya sana, nilichanganyikiwa sana kwani mambo waliyokua wanayafanya hata mimi Mama yao nikua sijawahi kuyafanya. Mwanangu wa miaka 12 alishaanza mapeni muda mrefu.

Niliamua kutokuongea kitu, nilimchukua mwanangu na kumpeleka Hospitalini kupima kila kitu na hapo ndipo nilichanganyikiwa zaidi kwani baada ya kutoka mbali na kuwa alikua tayari kashafanya mapenzi lakini alikutwa kashaambukizwa UKIMWI, nilichanganyikiwa, mume wangu alipandisha hasira ttulirudi nyumbani nikijua kuwa atamuua yule binti.

Nibiti ambaye alikua kama mwanangu nikimchukua kwao tangu akiwa na miaka 14 mpaka sasa ana miaka 17, nimeishi naye miaka mitatu na bado anaonekana kama mtoto. Tulirudi nyumbani na nilijaribu kumtuliza mume wangu kwani kwa hasira zake angemuua na ingekua kesi nyingine. Kwa utulivu tulimuita na baadaya kuongea naye aliamua kuongea ukweli.

Hapo ndipo nilichanganyikiwa zaidi kwani nilimuona mume wangu akiwa mkimya ghafla, binti aliniambia kweli ana UKIMWI na aliamua kutembea na mtoto wetu kama kulipa kisasi kwani alikua ameambukizwa ugonjwa huo na mume wangu, mume wangu alimbaka. Nguvu ziiliniishia nilimuambia muongo lakini nilipomgeukia mume wangu nilijua kweli amefanya kile kitu, nilishindwa hata kunaynyua mdomo na sijui nifanye nini?

SWALI NI JE INGEKUA WEWE UNGEFANYA NINI?

#IddMakengo
Next Post Previous Post
Bukobawadau