Bukobawadau

VODACOM YAJA KIVINGINE,YAZINDUA PINDUA PINDUA UNITS


Katikati Mwenye Kofia Ni Mkurugenzi Wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao Akiwa Na Timu Ya Vodacom Wakati Wakuzindua Pindua Pindua Units Mbele Ya Wafanyakazi Wa Vodacom Katika Ofisi Za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam


Na Dickson Mulashani
Mtandao wa simu wa Vodacom umezindua huduma mpya kabisa ya matumizi iitwayo PINDUA PINDUA UNITS ambapo imesheheni  ofa lukuki ikiwemo Whatsapp na Facebook bure huku upekee wake ni namna mtumiaji anapoweza kubadili matumizi ya units kulingana na uhitaji wake kwa wakati huo.

Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hii, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Bidhaa Vodacom Bi. Nandi Mwiyombella amesema PINDUA PINDUA UNITS imekuja kuleta mapinduzi ya huduma kwa watumiaji wa huduma za kimawasiliano kwani inampa mteja uhuru wa kutumia dakika na Mb kivyovyote.

Naye Mkurugenzi wa Vodacom Bw. Ian Ferrao alipongeza jitihada hizi na kusema hili ni miongoni mwa huduma ya ubunifu zaidi na ya kipekee kuwepo hapa nchini huku akitoa rai kwa vijana pamoja na watumiaji wa mtandao kuchangamkia fursa hii adimu kufanya mawasiliano yanayowezesha mabadiliko kadiri ya uhitaji.

Jinsi ya kujiunga na Pindua Pindua Units ni Kubonyeza *149*01# kisha kuchagua namba sita ambapo ni Kifurushi cha PINDUA PINDUA UNITS na kuwa huru kujiunga na units za ujazo wako ikiwa ni siku,wiki au mwezi.

"Nawasihi watumiaji wa Vodacom kuitumia fursa hii adimu kabisa na vile vile niwashauri wasiotumia mtandao wetu wajiunge ili waonje ladha kamili ya matumizi ya dakika pamoja na MB inayopatikana katika PINDUA PINDUA UNITS." alihitimisha Bi Nandi Mwiyombella.

Kwa Maelezo Kuhusu Pindua Pindua Angalia Video Hii.
Mkurugenzi wa Vodacom Bw. Ian Ferrao akifuatilia jambo wakati wa shughuli ya uzinduzi wa  Pindua Pindua Units Mbele Ya Wafanyakazi Wa Vodacom Katika Ofisi Za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam

Baadhi ya wafanyakazi pamoja na wadau waliohudhuria shughuli ya uzinduzi wa huduma ya Pindua Pindua Units katika ofisi  za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam

TUMEWEZAAAAAAA!!!!!!!! Wafanyakazi wa Vodacom wakifurahia mafanikio ya huduma hii ya kipekee ya Pindua Pindua

Wafanyakazi wa Vodacom wakijfurahia huduma ya Pindua Pindua Units wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo  katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es salaam

Next Post Previous Post
Bukobawadau