Bukobawadau

BENKI YA AZANIA YAENDELEA NA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTEMBELEA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)

Na Mwandishi Wetu.
Benki ya Azania leo imeendelea na Maadhimisho ya  Wiki ya huduma kwa Wateja kutembelea Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ambapo imekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba.

Akizungumza ofisini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe amesema kuwa wameitembelea TCRA kutokana na kuwa Wateja wao wakubwa wanaowathamini.

Itembe amesema kuwa wanaendelea kutembelea Wateja wao Bega kwa Bega ili kuwahudumia vizuri, pia kusikiliza maoni yao juu ya huduma zinazotolewa na Benki hiyo zikiwemo changamoto pamoja na ushauri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba ameshukuru kutembelewa na Benki ya Azania, ambapo amesema kuwa wamefurahi kutokana na kuwa Wateja wa Benki hiyo. Mhandisi Kilaba amesema kuwa wao kama TCRA hawajakosa pa kwenda isipokuwa huduma zilizopo kwenye benki hiyo zinawafaa. Pia ameiomba Benki ya Azania kuwekeza kwenye viwanda ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Pia amesema Watumishi wa Malamka hiyo hawajapata vikwazo kupata huduma kama Taasisi katika Tawi hilo lililopo Mawasiliano.

Hata hivyo, Mhandisi Kilaba ameishauri Benki hiyo kuwa na ubunifu zaidi katika sehemu nyingi, kuboresha mambo kama ya Mobile Bank ili kuwafikia wateja wengi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba(wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(Wa pili kulia), Meneja wa Tawi la Benki la Azania la Mawasiliano, Valentina Chamasa, Meneja Mkuu wa Benki ya Azania, Nyansaho Rhimo( wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Alinanuswe Kabungo(wa tatu kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati(kushoto).

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimshukuru mkurugenzi kwa niaba ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuwa wateja wao wa muda mrefu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuwa wateja wa benki hiyo ili kupunguza adha kwa wafanyakazi hao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akizungumza kuhusu namna benki ya Azania inavyoweza kujikita kusaidia kukuza viwanda hasa vidogo vidogo na vikubwa ili kuendana na kazi ya Rais Magufili kufikia kwenye malengo waliyojiwekea kama taifa pamoja na kuwashauri kupanua huduma hasa kupitia njia ya simu ili kuwafikia wateja wengi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
Meneja Mkuu wa Benki ya Azania, Nyansaho Rhimo(kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Alinanuswe Kabungo(wa pili kushoto) wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi alipokuwa anakabidhiwa hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) kuhusu namna wanavyofanya kazi bega kwa bega na wafanyabiasha wa Kariakoo kwenye moja ya duka la wateja wa Benki ya Azania  walipowatembelea leo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau