Bukobawadau

HAFLA YA UZINDUZI WA TAWI JIPYA LA NMB KAITABA MANISPAA YA BUKOBA

 Benki ya NMB yazindua tawi jipya katika Manispaa ya Bukoba ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma zake kwa wateja wa benk hiyo. Tawi jipya la Benki ya NMB lijuliknalo kwa jina la KAITABA lilizinduliwa Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Oktoba 4, 2017.
Katika uzinduzi huo wa tawi jipya la Kaitaba pia Mkurugenzi wa NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker alihudhuria ambapo alisema kuwa tangu kubinafsishwa kwa Benki ya NMB miaka 12 iliyopita tawi la Kaitaba ni tawi la 211 kutoka matawi 100 yaliyokuwepo awali nchi nzima.
Bi Ineke alisema Benki hiyo imepiga hatua kubwa za kimaendeleo tangu kubinafsishwa miaka 12 iliyopita kwani hadi sasa Benki hiyo ina Mawakala zaidi ya 3800 nchi nzima. Aidha alisema kuwa tayari Benki hiyo inatoa huduma za internet kuwa wateja wao ambapo wanaweza kutoa fedha popote walipo bila kufika katika Benki.
 Muonekato wa Jengo Jipya la Benki ya NMB Tawi la Kaitaba lililopo Mjini Bukoba.
Pia Bi Ineke Alisema kuwa Benki ya NMB tayari ipo kwenye soko la hisa na hisa zake zinapanda kila siku pia tayari hisa hizo zina wateja zaidi ya milioni 2. “Benki ya NMB kwasasa ni benki bora afrika na tumepata cheti cha ubora .” Alisistiza Bi Ineke.
Aidha, Bi Ineke alitoa ufafanuzi wa kwanini limeongezwa tawi jipya katika Manispaa ya Bukoba kuwa ni kutokana na maombi ya wateja wao kuwa hapo awali huduma zilikuwa haziendi kama matarajio ya wateja wao na wao kama benki wakaamua kutekeleza maombi ya wateja kwa kuongeza tawi la Kaitaba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akizindua tawi la Kaitaba aliwashukuru Uongozi wa Benki ya NMB kuongeza tawi jipya mjini Bukoba na aliwaasa wajasiliamali kutumia fursa hiyo kuongeza mitaji yao kupitia Benki ya NMB tawi la Kaitaba.
Aidha, Mhe Kijuu alitoa wito pia kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera hasa Manispaa ya Bukoba kuchangamkia huduma ya chap chap iliyoanzishwa na Benki ya NMB ili kupata huduma za kifedha kwa wakati na kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.
 Kaimu Afisa wateja Binafsi wa Bank ya NMB (Acting CRB)  Abdul Majid akitoa neno na kuwakaribisha waalikwa walioshiriki hafla ya Uzinduzi wa Tawi Jipya Kaitaba Manispaa Bukoba
 Wadau wakifatilia kinachojiri.
Kijana na ujasiriamali

Muendelezo wa Matukio yaliyojiri katika hafla ya Uzinduzi wa Tawi la NMB Kaitaba Mjini Bukoba leo Oct 4,2017
Sehemu ya Maofisa wa Bank ya NMB kutoka makao Makuu wakifatilia kinachojiri
 Muendeleozo wa matukio ya picha katika hafla ya Uzinduzi wa Tawi la NMB Kaitaba Bukoba
 Sehemu ya wadau wa NMB walioshiriki hafla hiyo
 Taswira mbalimbali eneo la tukio
 NMB Bank Tawi la Kaitaba Bukoba

 Mdu Divo Lugaibula pichani kushoto
 Bi Anitha Rugalabamu pichani .
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akikata utepe katika Uzinduzi wa Tawi la Kaitaba,pichani kushoto ni Bw.Protase Tehingisa Mkurugenzi wa bodi ya NMB ,kushoto ni  Bi Inke Bussemaker (MD)
 Baadhi ya maofisa wa Bank ya NMB Tawi la Kaitaba Bukoba
 Baadhi ya maofisa wa Bank ya NMB Tawi la Kaitaba Bukoba
Wasanii wa Kundi la Kapotive star singers-Bukoba
 Burudani ikiendelea kutoka kwa Wasanii wa Kundi la Kapotive star singers-Bukoba

Credit:Bukobawadaumedia
Next Post Previous Post
Bukobawadau