Bukobawadau

BUKENYA CUP 2017:Kamachumu Stend 1-1 Izigo Fc

Michuano ya kuwania kombe la #BukenyaCup2017 imeendelea leo Jumapili Nov 19,katika Uwanja wa Kalemela -Polisi Kamachumu kwa kuzikutanisha timu mbili zenye ushindani mkubwa Stend FC ya Mji Mdogo wa Kamachumu na Izigo Fc
Matokeo ni sare ya 1-1 bao la stend likifungwa na Mchezaji George Richard mnapo dk 78 kufuatia kazi nzuri ya mchezaji Irary Yunusu,Nao Izigo Fc wakapata kusawazisha bao hilo dakika chache baadaea kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri Beranus Khalid aliyeweza kuunganisha  mpira wa Close kutoka kwa winga machachari Jamiry Juma ikiwa ni dk 89 ya mchezo huo.

 Mgeni wa heshima OSC Angelo wa kituo cha kamachumu akitoa nasaha kwa timu zote mbili
 Wachezaji wa Timu ya Stend Fc ya Kamachumu
 Wachezaji wa Timu ya Izigo Fc.
 Mgeni maalum Mzee Geoge Lugakingira akiongozana na mgeni Rasmi kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili zinazokutana jioni ya leo Nov 19,2017
 Mzee Geoge Lugakingira ambaye ni Afisa mtendaji Kata Kamachumu akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
 Manahodha wa timu zote mbili katika picha na waamuzi wa mchezo huo
 Mashabiki wa Soka wakiwa tayari kushuhudia mpambano huo wenye lengo la kudumisha Ujirani mwema kwa udhamini mkubwa wa Mdau Ibrahim Bukenya
 Tayari mpambano umeanza Uwanjani  kati ya Stend Fc na Izigo Fc
 Anaonekana Mzee Kabarabara pichani,Mdau mkubwa na mlezi wa Soka kata Kamachumu
 Hakika mchezo huu umegusa hisia za watu wengi
 Beki mahiri wa Izigo Fc akiwajibika uwanjani
 Mdau Mohamed Kassim pichani
Pichani kulia ni Mh. Diwani Danstan akifuatilia mtanange huo
 Taswira kutoka wanja wa Kalemela -Kamachumu,
 Sehemu ya mashabiki wakifuatilia mtanange huo jumapili ya leo Nov 19,2017 Michuano ya #BukenyaCup
 Taswira mbalimbali Uwanjani, mtanange ukiendelea
  Sehemu ya mashabiki wakifuatilia mtanange huo jumapili ya leo Nov 19,2017 Michuano ya #BukenyaCup
 Taswira mbalimbali Uwanjani, mtanange ukiendelea


 Michezo ni Utamaduni mzuri katika Jamii,Michezo ni furaha, michezo ni Afya, michezo ni Umoja
 Hao ni wanazi wa Soka kutokapande hizi za Mji mdogo wa Kamachumu

 Endelea kufatilia matukio ya picha kupitia mtandao wako pendwa wa #bukobawadau
 Mtanange ukiendelea kutoka Uwanja wa Kalemela -Polisi Kamachumu
 Sehemu ya mashabiki Uwanjani
 Patashika Uwanjani kama unavyoweza kujionea kupitia picha,miamba miwili ikiendelea kuchuana
 Michezo ni Utamaduni mzuri katika Jamii,Michezo ni furaha, michezo ni Afya, michezo ni Umoja
 Muendelezo wa matukio ya picha Uwanja Stend Fc Uso kwa Uso na Izigo Fc
 Mlinda Mlango Varelian Delphinius wa Stend Fc ya Kamachumu
 Watu juu ya mti wakifuatilia Soka
 Sehemu ya wapenzi wa Soka wakiendelea kufuatilia kinachojiri ni michuano ya #BukenyaCup2017

  Kona ikipigwa kuelekea lango la timu ya Izigo FC
 Mpaka mapumziko Stend Fc 0 - 0 Izigo Fc
 Winga Wa Izigo Fc Jamiry Juma akielekeza shambulizi kwa timu pinzani
 Mlind mlango wa Izigo Fc Yasini Issa akianzisha mpira
 Wachezaji wa Stend Fc wakishangilia bao lililofungwa na Mchezaji George Richard
 Dakika ya 78 Stend Fc 1-0 Izigo
 Dakika za lala salama Izigo Fc wanasawazisha kupitia kwa mchezaji Beranus Khalid, Stend 1-1 Izigo
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Uwanja wa Polisi Kamachumu #Stend 1 #Izigo 1
Next Post Previous Post
Bukobawadau