Bukobawadau

MATUKIO YA PICHA HITIMISHO KONGAMANO LA #AzimioLaKagera

 Hatujahitimisha bado huu ndiyo mwanzo hatuwezi kuishia hapa tukaliacha kama Tamko sisi kama CMG tutalibeba kama Azimio kufika mwisho. Tumezunguka zaidi ya miaka 5 tumesikia vilio vinavyofanana kwa Vijana kabla hatujakwenda mbele lazima tufanye kitu kikubwa kwa ajili ya historia ya nchi hii. Jana tumeanza kwa kujiuliza Kwa swali Je tunaimba wimbo mmoja kwa Sauti zenye kufanana? Inawezekana hadi tunaondoka hapa bado hatujapa Sauti moja Lakini naimani tutafikia lengo. 
Tunaposema anzia sokoni lazima tuangalie Uongozi wa kimasoko namna gani tunaweza kushindana pasipo kushushana kwenye mazingira ya ushindani, Ubakie kwenye maneno tu na Vitendo vionekane Sokoni. Hebu tujaribu kutafuta taarifa na lazima wote tukubaliane kusaidia na maafisa kilimo na viongozi katika kuodoka katika Kilimo cha Kisasa. Sababu kilimo chetu kimepitwa na wakati. Kama tuna uwezo wa kupata mifumo bora zaidi katika huduma za kijamii tujipe Moyo na wala tusivutane kama kuna Fursa zipo tuzikimbilie katika kuzalisha huduma bora zaidi. Misingi yetu lazima ijikite katika namna ya kusolve tatizo bila kulalamika, Malalamishi tunayoishi nayo yageuke kuwa changamoto ambazo ni fursa kwetu tutengeneze kitu kinachoitwa Problem Solving Skills. Ndani ya Mwezi mmoja unaofuata kuanzia sasa kupitia WAMANTA waliopo hapa, Watu wa kwenye mitandao pamoja na wengine walio pamoja nasi tutatengeneza timu kwa ajili ya andiko la Azimio la Kagera. kabla ya Bunge la bajeti 2017/18. Hili #AzimioLaKagera Leo kwa pamoja tumeandika historia kubwa sana namshukuru mwenyezi Mungu kupata viongozi wa dini ambao tumeshindana nao kuanzia siku ya Jana hadi leo ni faraja kwetu. Kwasisi tuliobahatika kuishi leo lazima tubadilishe mtazamo wa kuitengeneza Kagera mpya yenye mtazamo mpya kama mipaka ya kiuchumi na siyo eneo la Ulinzi wa mipaka yetu. 
Muasisi wa Fursa
Ruge Mutahaba.
#AzimioLaKagera
 Huwezi kumdhibiti mwanamke, sababu Mwanamke anatumia akili Kwa asilimia 10 na asilimia 90 zilizobaki hawatabiriki. Dkt. Elly #AzimioLaKagera
 Sehemu ya watoa mada  #AzimioLaKagera
 Wadau wakifurahia mijadala inayoendelea
Nafasi ya kushinda ipo kwa kila anayejaribu kupambana na kutoka nje ya mipaka na mazoea ya kawaida. Muasisi wa Fursa ndugu Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Fursa @sumamwaitenda wakifurahi Experience story za mchokoza mada katika sekta ya Creative Industry #KingMsukuma
 Mwenyekiti wa 'Tugaruge' Mr Ben Mulokozi akifatilia mada zinazoendelea katika kongamano la #AzimioLaKagera,kulia kwake ni Muasisi wa Fursa ndugu Ruge Mutahaba
 Nawashukuru sana Clouds kwa kutekeleza agizo la Mh. Rais JPM alilololitoa akiwa jimboni mwangu na mimi binafsi tayari tarehe 14/12/217 kupitia mkutano wa wadau tumezindua Mkakati wa kuimarisha soko la Haki kwa maendeleo ya Wakulima wa kahawa mkakati wenye lengo la kuongeza pato la mkulima wa kahaa na kuongeza kasi ya maendelea #BaloziDtkKamala # MbungewaNgenge 
Mpango huo unalengo la kumwezesha mkulima wa kahawa kutamba viwango vya ubora wa kahawa katika soko la biashara ya haki  #AzimioLaKagera

Wadau mbalimbali wakiendelea kuchangia mijadala  #AzimioLaKagera


 Taswira ukumbi wa ELCT Bukoba Hotel #AzimioLaKagera

 Mkurugenzi wa Fursa @sumamwaitenda akiongoza mada inayoendelea  ukumbini 
Kinachokosekana hapa ni Elimu ya Ugani, Pembejeo na uwezeshaji tatizo hakuna Benki inayokopesha wakulima katika AgroProcessing ipo Benki ya Kilimo lakini bado sana na malengo yetu baada ya miaka 5 tuzalishe tani laki 5 za Kahawa. Kama tukitilia mkazo kwenye Kilimo cha Kahawa Kagera itasonga mbele. #AmiriHamza #AzimioLaKagera


Katika Kilimo cha Tanzania baada ya Uhuru tulitegemea kilimo kuendesha Uchumi kupitia (Katani, Tumbaku na Kahawa) hali ni tofauti na sasa kabisa. Hali imebadilika tumeshindwa kuendana na mahitaji ya sasa au Vijana wa leo wamechoka? 
Kama tuliweza kufanya Uhakiki wa idara za serikali kubaini wafanyakazi hewa na wasiokuwa na vyeti na sifa stahiki! Kwanini tusigeukie kwenye kilimo kufanya uhakiki wa kubaini kuna asilimia ngapi ya Watanzania ni wakulima? Maarifa na Teknolojia tunayo ya kufanya kilimo cha Kisasa.. Tuamue kuwa serious tunaweza kufanya mageuzi katika kilimo cha sasa kuwa Kilimo biashara. #AvityBuchwa #AzimioLaKagera

Mwisho wa matukio 
#AzimioLaKagera
Next Post Previous Post
Bukobawadau