Bukobawadau

MKAKATI WA KUIMARISHA BIASHARA YA HAKI KWA MAENDELEO YA MKULIMA WA KAHAWA WAZINDULIWA RASMI NA MBUNGE WA NKENGE BALOZI DKT.DIODORUS KAMALA - ''FAIRTRADE STRATEGY FOR COFFEE GROWERS PROSPERITY''

Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala  Mbenge wa Jimbo la Nkenge  siku ya jana kupitia mkutano mkubwa wa wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge ameweza kuzindua rasmi Mkakati mahususi wa Kuimarisha Biashara ya haki kwa maendeleo ya mkulima wa  Kahawa ''Fairtrade Strategy for Coffee Growers Prosperity'' Lengo kuu la Mkakati huo ni kuongeza pato la mkulima wa kahawa na kuongeza kasi ya maendeleo kwa kuongeza uzalishaji wa kahawa na tija,kumwezesha mkulima wa kahawa kutambua viwango vya ubora wa kahawa katika soko la biashara ya haki,kuongeza bei ya kahawa anayopata mkulima na kupunua mtandao wa wadau wa biashara ya haki.
Akiongea na wadau waliohudhuria mkutano huo unaofanyika kila mwaka na kuandaliwa na Mbunge mwenye, Balozi Dkt.Buberwa Kamala  amebahinisha vyama 26  vya Ushirika vya msingi katika Jimbo la Nkenge vitavyoshiriki kutekeleza  Mkakati wa Kuimarisha Biashara ya haki kwa maendeleo ya Mkulima wa  Kahawa ,eneo la Ardhi linalolimwa kahawa Wilayani Missenyi ,Wilaya yenye hekta za ardhi  270,875 ,kati ya hizo  hekta 105,298.4 zinafaa kwa kilimo na ardhi ambayo ina mazao ni hecta 53,532 ambayo ni asilimia 50.8 inayofaa kwa kilimo na kwa maana hiyo ardhi bado ipo amesema; Balozi Dkt Kamala
Balozi Dkt.Buberwa Kamala amewaelezea wadau Uwezo wa Wilaya ya Missenyi katika uzalishaji wa kawaha : Historia ya uzalishaji wa Kahawa ,BCU na Elimu ya Kagera,Sosial Premium kuanzisha kilimo hai,Hisa za Wakulims kwenye kiwanda cha TANICA kutoka asilimia 7 hadi asilimia 53.Shilingi za Kitanzania milioni 800 zimtumika kutokana na kuuza kahawa kwenye soko la Haki,Kununua mitambo mipya ya kukoboa kahawa kwenye kiwanda cha BUKOP pamoja na marekebisho ya kiwanda 1.4 bilioni zimetumika,kuboresha maghala ya vyama vya msingi, kuwekeza kwenye majengo ya kitega uchumi,kuwepo kwa mtandao wa vyama vya ushirika vya msingi,Uwepo wa ardhi ya kutosha, hali ya hewa na mvua za kutosha na uwepo wa wakulima wa kahawa wenye uzoefu na zao la kahawa
Pamoja na haya Mh. Mbunge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala  ameelezea udhaifu uliopo katika uzalishaji wa Kahawa Wilayani Missenyi ikiwa ni pamoja na: 

-Kutozingatia uzalishaji bora wa Kahawa
-Kutoanzisha mashamba mapya  ya kahawa
-Kutokuanzisha Vitalu vya Miche vya kutosha
-Kodi na Ushuru mbalimbali katika kahawa
-Miundombinu dhaifu ya kusaidia soko la kahawa


Fursa zilizopo katika uzalishaji wa Kahawa ni pamoja na :
-Kuwepo kwa Soko la Fairtrade (Minimum Price  na Social Premium)
-Uwezekano wa kuongeza Soko la ndani la wanunuzi wa Kahawa
-Kuwepo kwa waumini wazuri wa biashara ya haki
-Utayari wa Serikali kusaidia wakulima wa Kahawa (Kodi 18 zimefutwa na nyingine zitafuata
Mwenyekiti wa Halmashari ya Wilaya Missenyi Projestus Tegamaisho akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano wa Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Nkenge uliofanyika Jana katika ukumbi wa Halmshauri Missenyi-Bunazi
Wadau waliohudhuria mkutano huo wakifatilia Somo kutoka kwa Mbunge wao Balozi Dkt Diodorus Buberwa Kamala
Ambapo pia Mh .Mbunge Balozi Diodorus Buberwa Kamala ameelezea kwa kina changamoto zinazokabili uzalishaji wa kahawa ambazo ni:
-Kuwepo kwa wanunuzi maarufu kwa jina la Balimanya ila! yaani 'Wajuuzi wajanja wajanja'
-Bei za kahawa zisizoridhisha
-Biashara ya kununua kawaha changa 'Butura' Kushamili
-Ununuzi wa Kahawa mbichi kushamili
-Mabadili ya tabia nchi
-Kuacha kutumia mizani ya KCU ya asili
-Kutozingatia kwamba uongozi na utendaji kwenye vyama vyama vya ushirika ni kwa manufaa ya wanachama na si kwa ajili ya watu binafusi
Inaendelea....Wilaya ya Missenye ipo kilomita 150 kusini mwa Equator,Kaskazini Wilayavya Missenyi inapakana na nchi ya Uganda,Magharibi inapakana na Wilaya ya Karagwe na kusini inapakana na Wilaya ya Bukoba, Upande wa mashariki wa nchi kavu wa Wilaya ya Missenyi kunaziwa victoria,Wilaya ya Missenyi ina njia kuu ya kuelekea Uganda,Sudani ya Kusini,Kenya, Rwanda na Burundi.
Kwa maneno mengine Wilaya ya Missenyi ni njia kuu ya Tanzania ya kuingia Afrika Mashariki (Tanzania East Afrika Gateway)
TAZAMA KATIKA VIDEO HAPA CHINI YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA WADAU
Hivi ndivyo Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala alivyozindua rasmi mkakati wa kuimarisha biashara ya haki kwa maendeleo ya wakulima wa kahawa.
Fairtrade strategy for coffee growers prosperity
Fairtrade for Farmers,fairtrade for Nations''
Next Post Previous Post
Bukobawadau