Bukobawadau

PICHA:MAZISHI YA ASKOFU NESTOR TIMANYWAAnaandika Baba Askofu Kilaini;Mpendwa Baba Askofu Nestor Timanywa,Wakati tunaomboleza kifo chako tunamshukuru Mungu ambaye alitupa zawadi ya baba mwema kama wewe. Ulikuwa mpole, ulimjali kila mmoja na hukutaka mtu aumie bure bila sababu. Ulikuwa mnyenyekevu na kila mmoja aliweza kukufikia bila shida. Ulikuwa mcheshi mwenye michapo mingi kiasi kwamba maaskofu wote hata wale wadogo walikutania wakikuita “Ora Pro Nobis”.

Hata ulipokuwa mgonjwa unateseka hukulalamika hata siku moja; ulipokea ugonjwa na maumivu kwa imani kubwa. Umeliongoza jimbo la Bukoba kwa miaka 39 kwa upendo mkubwa. Sote tuliofanya kazi chini ya uongozi wako tunakulilia na kukuombea raha ya milele mbinguni.
Kwa heri Baba yetu Timanywa

Maaskofu 22 wanashiriki ibada ya mazishi ya Askofu mstaafu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Nestor Timanywa itakayoongozwa na Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam Thadeus Ruwai'ichi.
Mazishi yanafanyika katika kanisa la Bikra Mariam, Mama Mwenye Huruma mjini Bukoba ambapo baada ya kuuaga mwili maaskofu na mapadri wameingia kanisani kwa maandamano.

Ndani ya kanisa ilipotengwa nafasi ya viongozi wa Serikali anaonekana mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti na baadhi ya wakuu wa wilaya.

Baadhi ya waumini wanafuatilia ibada hiyo wakiwa nje kwenye viwanja vya kanisa kupitia kwenye vipaza sauti na televisheni.
Marehemu Askofu Nestor Timanywa alifariki Agosti 28 mwaka huu wakati akitibiwa Hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Katikati ni Mkuu waMkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akitoa heshima za mwisho kuuaga Mwili wa Baba Askofu Nestor Timanywa
Bukobawadau Media tunatoa pole kwa Baba Askofu Rwoma, Askofu Msaidizi Method Kilaini, Mapadre, Watawa na Waamini wote.
#PumzikaBishopTimanywa
#MwendoUmeumaliza
#bukobawadau
Next Post Previous Post
Bukobawadau