Bukobawadau

BALOZI DR KAMALA KATIKA MKUTANO WA WADAU WA MAENDELEO YA JIMBO LA NKANGE 2019


Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwahutubia wadau waliohudhuria Mkutano wa wadau wa maendeleo ya Jimbo la Nkenge uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashaui ya Missenyi tarehe 3/01/2019.

Hotuba katika Mkutano wa Wadau

Waheshimiwa Wadau!

Ninayo furaha kubwa kuwakaribisha leo hii kushiriki Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya Jimbo la Nkenge. Karibuni sana na ahsante sana kuhudhuria.
Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana hapa leo hii.

Waheshimiwa  Wadau!
Naomba niwatakie  heri ya mwaka mpya. Kama mnavyofahamu mwaka huu umeitwa  Birug’omumpiita. Jina la mwaka huu linaenda sambamba na falsafa ya Hapa Kazi Tu! Kikao chetu cha leo kitatusaidia sana kuweka mipango na kubainisha vipaumbele vya kuzingatia kusukuma gurudumu la maendeleleo
Waheshimiwa Wadau!
Kama mnavyofahamu mwaka jana katika Wilaya yetu walizaliwa Watoto mapacha  Anisia na Marines waliokuwa wameungana. Baada ya taarifa hizo kuandikwa katika vyombo vya habari, Serikali ya Saudi Arabia iliamua kuchukua jitihada za makusudi za kufanya upasuaji wa kutenganisha Watoto hao. Tarehe 23/12/2018 upasuaji huo ulifanyka huko Saudi Arabia kwa mafaniko makubwa. Upasuaji huo hulijumuisha Madaktari Bingwa 32 na  wauguzi 120. Upasuaji huo ulioneshwa katika vyombo vya habari na ulichukua masaa 13. Nachukua fursa hii kumshukuru mfalme wa Saudi Arabia kwa kugharamia upasuaji huo uliogharimu wastani wa fesha za Kitanzania bilioni moja na milioni mia tano. Aidha, namshukuru pia Balozi wa Tanzania Saudi Arabia, Balozi Hemed kwa kuratibu na kuhakikisha upasuaji huo unafanikiwa.
Nawashukuru pia Madaktari na Wauguzi wote wa hapa Tanzania kwa huduma zao zilizowesha kuwandaa Watoto waliokuwa wameungana na hatimae kuwezesha upsuaji huo kufanyika. Vilevile nawakukuru Watanzania na Wanankenge kwa sala zenu zilizowezesha kufanikiwa kwa upasuaji wa mapacha hao.

Waheshimiwa Wadau!
Lengo kuu la mkutano huu ni kujadili maendeleo ya Nkenge na kuweka mikakati ya kusukuma gurudumu la maendeleo.  Katika kikao cha Wadau kilichotangulia kabla ya hiki   tulijadili na kupitisha Mkakati wa Kuimarisha Soko la Haki la Kahawa (Far Trade)  kwa Maendeleo ya Wakulima wa Kahawa Wilayani Missenyi. Baada ya kikao chetu, Serikali ilitoa msukumo mkubwa katika kuimarisha na kuendeleza zao la kahawa. Pia kwa mara ya kwanza, Serikali imeelekeza mnada wa kahawa uwe unafanyika hapa Kagera. Ni matarajio yangu maelekezo ya Serikali yatasaidia sana kuimairsha zao la kahawa. 

Waheshimiwa Wadau!
Katika kikao chetu cha leo tutatathimini mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika miaka mitatu kuanzia mwaka 2016, 2017 hdi 2018.   Pia tutabainisha maeneo ya kuongeza msukumo katika kuharakisha maendeleo ya Jimbo letu la Nkenge.


Waheshimiwa Wadau!
Kama mnavyofahamu mgogogro wa mipaka kati ya Ranchi ya Missenyi na vijiji vinavyopakana na Ranchi hiyo umechukua muda mrefu. Manamo tarehe 10/05/2018 nilimuandikia Mhe. Waziri Mkuu na kumuomba asaidie kumaliza mogogoro huo. Mhe. Waziri Mkuu amaechukua hatua muhimu za kusaidia kumaliza mgogoro huo. Maelekezo yametolewa kwa Wizara zote zinazohusika na mgogoro huo na ni matarajio yangu tutapata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.

Waheshimiwa Wadau!
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Bajeti 2017/18 lilishauri kuwa kuwa migogoro yote ya mipaka ya hifadhi na wananchi itaamuliwa kwa ushirikishwaji wa wadau wote muhimu wakiwepo viongozi wa Serikali, wanasiasa, wananchi na taasisi zinazohusika na uhifadhi. Aidha, Mkurugenzi wa Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi ndiye mwenye dhamana ya kisheria ya kuonesha mipaka yote ya Ardhi nchini iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria. Ni matarajio yangu kuwa ushauri wa Bunge kwa Serikali utatusaidia sana kupata ufumbuzi wa kumaliza igogoro ya mipaka kati ya Msitu wa Minziro na vijiji vinavyozunguka msitu huo na pia tutapata ufumbuzi wa  na wa migogoro ya mpaka kati ya Hifadhi za Taifa za Rusiina, Kiikuru na vijiji vinavyozunguka hifadhi hizo.

Waheshimiwa Wadau!
Mojawapo ya kazi muhimu za Bunge ni kutunga sheria. Hivi karibuni kuna miswada mitano ya sheria ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Muswada ukisomwa kwa mara ya kwanza bungeni unatoa fursa kwa wadau kuanza kutoa maoni yao. Natoa wito kwa wadau wa maendeleo ya Nkenge kusoma miswada hiyo na kunipatia maoni yenu ili wakati wa kutunga sheria ukifika niweze kuwasilisha maoni yenu.
·        Miswada hiyo ya sheria ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza ni Pamoja na: Muswada wa Sheria na 4 wa madailiko ya Sheria Mbalimbalimbali, 2018
Muswada huu unalenga kufanya mabadilko katika Sheria ya Serikali za mitaa,\
·        The Tanzania Meteorological Authority Bill, 2018
Muswada huu unalenga kuanzisha wakala wa kuratibu hali ya hewa. Pamoja na mambo mengine muswada huu unabainisha adhabu zitakazotolewa kwa makosa mbalimbali kwa wale watakaovunsja sheria husika. Sheria hii itanya kazi Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
·        The Land Transport Regulatory Authority Bill, 2018
Muswada huu utaanzisha Wakala wa Usafiri katika nchi kavu
·        The Politica Parties (Amendments Bill, 2018 na
·        The Water Supply and Sanitation Bill, 2018
Taarifa ya Mafanikio

Miswada niliyobainisha hapo juu inapatikana mabadiliko zinapatikana katika tovuti ya Bunge inayopatikana katika anwani parliament.go.tz

Waheshimiwa Wadau!
Kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 kuna mafanikio mengi yaliyotokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM. Katika Mkutano huu wa Wadau naomba nitaje baadhi ya mafanikio ya yaliyotokana na utelekezaj wa Ilani ya CCM katika ngazi ya Halmashauri ya Missenyi
Jedwali na II: Baadhi ya Mafanikio ya Utekelezaji wa ilani ya CCM katika Ngazi ya Halmashauri ya Wiilaya ya Missenyi

Na.
Mafanikio
Matarajio
1.      
Asilimia ya upatikanaji dawa imeongezeka kutoka asilimia 68 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 92 mwaka 2017/18
Bado kuna baadhi ya dawa ambazo haziko kwenye kundi za dawa mahimu. Zinakosekana kwenye vituo vya kutolea huduma.
2.      
Vituo vya kutolea huduma za afya 22 vimeboreshwa kwa kupaka rangi, kujebga vichomea tala na placenta  pit
Bado vijiji 45 havina zahanati na kata 17 hazina vituo vya afya
3.      
Ongezeko la wanachama mfuko wa afya ya Jamii CHF kutoka asilimia 8 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 30 2017/18
Kasi ndogo ya wananchi kujiunga na CHF. Kutekelezwa kwa chf iliyoboresha kutasaidia kuboresha huduma za afya
4.      
Jumla ya wazee 6,082 kati ya wazee 11,514 waliotambuliwa wamepewa vitambulisho sawa na asilimia 52.8
Wazee wote waliotambuliwa watapatiwa kadi za matibabu bure
5.      
Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kabyaile
Kuboresha huduma za kituo cha afya cha Kabyaile
6.      
Kiwango cha wagonjwa wa malaria kimepungua kutoka asilimia 17 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 12 mwaka 2017/18
Kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi bora ya vyandarua
7.      
Kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kimepungua kutoka asilimia 3.5 mwaka 2015 hadi asilimia 2 mwaka 2018
Kupunguza maambikizi mapya ya ukimwi na kuendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya ukimwi na kuwaanzishia dawa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
8.      
Kiwango cha utoaji chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 85 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 92 mwaka 2018
Kuhakikisha wote wanaostahili kupewa hanjo wanapata chanjo
9.      
Kupata milinioni 400 kutoka Serikali kuu za kuboresha kituo cha afya Bunazi
Kituo cha Afya Bunazi kuendelea kuboreshwa
10.  
Halmashauri kwa kushirikiana na Kituo cha  Utafiti Maruku imefanikiwa kusambaza miche bora ya kahawa 32,200 kwa wakulima
Mahitaji ya miche bora ya kahawa bado ni makubwa. Halmashauri itaanzisha vitalu
11.  
Kwa kutumia  mfuko wa Mbunge Halmashari iliweza kusambaza mbegu bora za Alizeti kilo 240 sawa na ekari 34 ili kuhamasisha kilimo cha Alizeti

12.  
Kuanzishwa kwa mazao mapya ya kilimo kwa nia ya kuongeza kipato cha mkulima. Mazao ya Alizeti, Chia Seeds na Soya yameanza kulimwa katika Wilaya ya Missenyi.

13.  
Halmashauri imeweza kufanya sensa ya wakulima wa kahawa na kupata jumla ya wakulima 14,264 waliolima jumla ya ekari 4,557 yenye miti ya kahawa aina ya arabika 22,018 na miche ya robusta 1,483,513

14.  
Kukamilika kwa mradi wa maji Kilimilile ambao umegharimu 400,000,000/=

15.  
Mradi wa maji Rukurungo umekemilika na umegharimu 424,547,000/=

16.  
Mradi wa maji Nyabihanga wa zisima vifupi viwli umekamilika na unafanya kazi kwa gharama ya 214,392,000/=

17.  
Mradi wa maji wa Igurugati umegharimu 290,297,244/=

18.  
Mradi wa Maji wa Kenyana kisima kirefu umegharimu 328,507,000/=

19.  
Mutukula mradi wa maji mradi umegharimu milioni 653,288,886

20.  
Bubale, Kibeo na Bwoki. Uchimbaji wa visima unaendelea.  Mradi umegharimu 142,602,665

21.  
Kakunyu mradi utakaogharimu 779,296,100/= unaendelea kujengwa

22.  
Bugango, mradi unaendelea kujengwa na utagharimu milioni 782,234,200/=

23.  
Ruzinga, Ruhija na Mgongo mradi utagharimu 314,047,681 unaendelea kujengwa

24.  
Mradi wa maji Kibeo ambao utagharimu 123,404,000/= unaendelea kujengwa








25.  
Mradi wa maji ya mto Kagera kwa ajili ya Kyaka na Bunazi. Maandalizi ya kuanza kutekeleza mradi yanaendelea. Mhandishi Mshauri mpya amaepatikana.  Kibali cha kuanza kazi kinasubiriwa kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

26.  
Kuongezeka vyumba vya madarasa kutoka 521 mwaka 216 hadi 650 mwaka 2018

27.  
Kuongezeka nyumba za walimu kutoka 192 mwaka 2016 hadi 205, mwaka 2018

28.  
Kuonezeka matundu ya vyoo kutoka 887 2016 hadi 915 2018

29.  
Madawati kuongezeka kutoka 15,269 mwaka 2016 hadi 19,786 mwaka 2018

30.  
Kiwango cha kufaulu darasa la saba kimeongezeka kutoka asilimia 78.8 mwaka 2016 hadi 83.7 mwaka 2018

31.  
Kiwango cha kufaulu darasa la nne kimeomgezeka kutoka asilimia 86 mwaka 2015 hadi asilimia 88 mwaka 2017

32.  
Ufaulu wa mitihani kidato cha pili umeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi asilimia 84.5 mwaka 2017

33.  
Ufaulu wa mitihani kidato cha nne umeongezeka kutoka asilimia 62 mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2018

34.  
Vyumba 31 kati ya 66 vya maabara vimejengwa na vinatumika


Jedwali namba II limebainisha baadhi tu ya mafanikio. Mafanikio mengine nimewaachia wadau wa maendeleo waweze kuyabainisha. Aidha, Meneja wa TANESCO  wa wilaya ya Missenyi atabainisha mafanikio katika sekta ya nishati, meneja wa TARURA Missenyi naye atabainisha mafanikio katika Sekta ya barabara na Meneja wa MSD atabainisha mafanikio katika upatiakanaji na usambazaji wa madawa katika Wilaya ya Missenyi. Aidha, Bomba la Mafuta kutoka Uganda kuelekea Tanga nalo litachangia sana katika kuongeza mapato ya Taifa na kukuza uchumi

Waheshimiwa Wadau!


Mojawapo ya ahadi niliyotoa ni kutafuta fedha za kutoa mafunzo maalum ya kuwawezesha vijana na akina mama kuweza kujiajiri. Naomba niwajulishe kwamba hatimae tumepata mdau ambaye atatoa mafunzo kwa vijana na akina mama wasio chini ya mia tano ili waweze kujiajiri na kuongeza fursa za kipato. Mafunzo haya yataanza kabla ya mwaka wa fedha wa 2018/19 kumalizika. Taarifa zaidi nitawajurisha mafunzo yakikaribia kuanza.

Waheshimiwa Wadau!
Ahsante sana kushiriki katika Mkutano huu wa Wadau wa Maendeleo ya Jimbo la Nkenge. Na sasa nawakaribisha kutoa maoni yenu yenye lengo la kubainisha mikakati mbalimbali ya kusaidia kuonegeza kasi ya maendeleo katika jimbo la Nkenge. Kwa Pamoja tunaweze! Ahsante sana kunisikiliza.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akikabidhi pump ya kusukuma maji  Bi Theopista John wa Kijiji cha Bugogora ,Balozi Kamala ametekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa kikundi cha 'Nkenge Youth Group',kikundi kinacho jihusisha na kilimo cha mbogamboga maeneo ya Bugorora kando kando ya mto Kagera.
Mdau wa maendeleo akimsikiliza kwa makini mbunge wake.
 Baadhi ya wadau wakiendelea kushiriki mkutano huo
 Ndugu Jovin Barongo Kaimu Meneja wa TARURA halmashauri ya Wilaya Missenyi
 Eng. Idd Makung'uto Kaimu Mhandisi Maji halmashaui ya Wilaya Missenyi
 Mh.Tegamaisho Mwenyekiti wa Halmashauri Missenyi.
 Katibu wa CCM Wilaya Missenyi Mama Mbohe katika picha na Mkurugenzi wa Halmashauri Missenyi
 Balozi Dr.Kamala akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya Missenye ,Mama Mboha.
 Mdau akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa Jimbo la Nkenge
 Muendelezo wa matukio ya picha Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Wa Jimbo la Nkenge.
 Taswira mbalimbali wakati mkutano ukiendelea
 Ndugu Dominic Lumato Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya Missenyi akiongea kuhusu mchakato wa usambazaji wa Umeme Vijijini REA unavyoendelea Wilayani Missenyi 
 Dr. Joachim Mchunguzi Mazima akiendelea kushiriki mkutano huo ulio andaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala
 Mzee Leopold Rwizabdekwe pichani Mkazi wa Kijiji Katendaguro Kata Bugandika 
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa MSD kutoka MSD -Muleba ,Bw. Masatu Kalendero
 Dr. Habasi Mganga Mkuu wa Wilaya Missenyi
 Mh.William Osward Rutta Diwani wa Kata Ishozi
 Ndugu George Rubaiyuka Joseph Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari halmashauri Missenyi akitolea hoja ufafanuzi kuhusu elimu.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Nkenge, Lengo ikiwa ni kutathimia shughuli za maendeleo na kubainisha masuala ya kupewa kipaumbele mwaka 2019.

Next Post Previous Post
Bukobawadau