MKUU WA MKOA KAGERA AJA NA KAMPEINI YA SIKU TATU YA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANWAKE KUTATUA KERO ZAO ZOTE ZA UNYANYASWAJI
Na: Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuwakomboa wanawake ambao wamehangaika kwa muda mrefu kwa matatizo ya kunyanyaswa kijinsia, kudhurumiwa ardhi, migogoro ya mirathi, na kutelekezewa watoto ambapo ametenga siku tatu kufanya kampeini itakayojulikana kama “Kampeini ya Msaada wa Kisherai Kwa Wanawake” kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao ndani ya siku tatu hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuwakomboa wanawake ambao wamehangaika kwa muda mrefu kwa matatizo ya kunyanyaswa kijinsia, kudhurumiwa ardhi, migogoro ya mirathi, na kutelekezewa watoto ambapo ametenga siku tatu kufanya kampeini itakayojulikana kama “Kampeini ya Msaada wa Kisherai Kwa Wanawake” kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao ndani ya siku tatu hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Gaguti akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake Juni 21, 2019 alisema katika mkoa wa Kagera kero nyingi ni za ardhi lakini pia wanawake wamekuwa wakipata matatizo makubwa upande wa ardhi, mirathi, kunyanyaswa kijinsia pia kutelekezewa watoto jambo ambalo linawafanya wengi wao kufika mara kwa mara ofisini kwakwe kuwasilisha malalamikoa yao.
Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa sasa ameamua kutenga siku tatu za Kapeini ya msaada wa Kisheria kwa wananwake kuanzia tarehe 27 hadi 29 Juni, 2019 kuwasikiliza wanawake na kutatua kero zao kwa kuzihusisha Idara na Taasisi zote za Serikali na zisizokuwa za Serikali zinazohusika katika usaidizi wa kisheria au zinazojihusisha na ustawi wa jamii.
“Badala ya mama kuja ofisini kwangu alafu niwaite wataalamu wa kunisaidi kusikiliza matatizo na kunishauri au kumtuma mama huyo kuangaika katika ofisi nyingine nimeamua kuwaleta Wataalam wote pamoja ili watoe utatuzi wa kero za wanawake kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na ushauri wa nini mwanamke au mama aliye na kero afanye nini ili kero yake lifike mwisho.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Katika Kampeini hiyo ya Msaada wa Kisheria kwa Kanawake Mkoani Kagera patakuwepo na Wanasheria zaidi ya 15 ikiwa ni pamajo na wanaotoka Shirika la MHOLA linalojihusisha na usaidizi wa kisheria kwa wanawake, Maafisa wa Polisi Kutoka Dawati la Jinsia, Maafisa Wapelelezi kutoka Jeshi la Polisi, Maafisa Kutoka TAKUKURU pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kuhakikisha kila kero imepatiwa ufumbuzi.
Kampeini hiyo ya siku tatu ya Msaada wa Kisheria kwa Wanawake itatolewa bure bila gharama yoyote na itafanyika Viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba tarehe 27 hadi 29 Juni, 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi kila siku kwa siku hizo tatu na itafanyika kwa mfumo wa kielektroniki ili kuweka kumbukumbu sahihi juu ya utatuaji wa kero za wananchi.
Wito wa Mkuu wa Mkoa Gaguti kwa wanawake Mkoani Kagera ni kujitokeza kwa wingi kuleta kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi lakini pia akina baba haswa wanaonyanyaswa kijinsia pia nao wanakaribishwa kusikilizwa ili kero zao zitatuliwe pamoja na mwananchi yeyeyote mwenye kero yake anaombwa kuwasilisha ndani ya siku tatu zilizotajwa ili zipatiwe ufumbuzi.