Bukobawadau

WENYEJI WATOLEWA MICHUWANO YA RWEGASIRA CUP INAYOENDELEA MJINI BUKOBA

Timu ya Rwegasira Fc Wenyeji wa Michuano ya #RwegasiraCup inayodhaminiwa na  Edward Emmanuel Rwegasira siku ya jana wameyaaga mashindano hayo hatua ya nusu fainali kwa kufungwa 2-1 na timu ya BMC inayomilikiwa na Manispaa ya Mji wa Bukoba
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mtanange wa Mashindano ya Rwegasira Cup yaliyoandaliwa na Mmoja wa Watoto wa Marehemu mzee Emmanuel Rwegasira aliyewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba.
 Wachezaji wa timu ya BMC Wakiomba dua kabla ya mtanange kuanza
Line up wa kikosi kikali cha Wachezaji wa timu ya Rwegasira Fc iliyoyaaga mashindano hayo.
Mechi hiyo imechezeshwa na Mwamuzi mwanadada Jonesia Rukiyaa pichani katikati.
Taswira kutoka viwanja vya Chuo cha Afya Kagemu Manispaa Bukoba
 Piga nikupige Uwanjani Mashindano ya Rwegasira Cup yaliyoandaliwa na Mmoja wa Watoto wa Marehemu mzee Emmanuel Rwegasira katika kumuenzi Baba yake aliyekuwa mpenzi wa mpira wa miguu
 Benchi la wachezaji wa timu ya BMC
 Benchi la wachezaji wa timu ya BMC
 Taswira mtanange ukiendelea Uwanjani...
Wadau wa soka wakicheck na Camera yetu.
  Pongezi za hapa na pale kwa Nyota wa Mchezo huo mchezaji wa timu ya BMC
 Uwanja unaripuka kwa shangwe na furaha kwa wachezaji na wapenzi wa timu ya BMC kufuatia Ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwegasira Fc
 Wanaonekana Wachezaji wa Rwegasira Fc wakiwa na nyuso zenye huzunicvf
Kutoka Viwanja vya Chuo cha Afya Kagemu Rwegasira Fc 1-2 BMc.
Next Post Previous Post
Bukobawadau