Bukobawadau

#BUKOBA ZIARA YA NDG JOANFAITH KATARAIA NA VIONGOZI WA UVCCM MKOA KAGERA

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith Kataraia na Viongozi wa UVCCM Mkoa Kagera waendelea Ziara ya kuimarisha Jumuiya na Chama Mkoa kwa kuendesha Operation simika bendera katika Mitaa mbalimbali na kuzungumza na vijana kwenye maeneo ya shughuli zao za kiuchumi
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith Kataraia na Mjumbe wa baraza kuu Uvccm Taifa Ndugu Fahami Matsawili kwa pamoja wakimkabidhi bendera kiongozi wa waendesha bodaboda maarufu kama Assecdo wa Kijiwe chae Hospitali Kuu ya Mkoa Kagera
Taswira eneo la Kijiwe cha waendesha bodaboda kilichopo nje ya Hospital ya Mkoa Kagera
Ndugu JoanFaith Kataraia Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa akitazama bendera ya CCM inavyopepea
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera Ndugu Happiness Runyogote akiongozana na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Uvccm Taifa Ndugu Joanfaith kataraia na Mjumbe wa baraza kuu uvccm Taifa Ndugu Fahami Matsawili kwa pamoja na Viongozi waandamizi wa UVCCM Manispaa Bukoba wakizungumza na Vijana wa stend kuu ya Mabas Mjini Bukoba.tulifanya ziara ya kuwatembelea vijana wenzetu vijiweni kwao kwa kuzungumza nao na kusimika bendera za chama chetu
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith Kataraia
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith Kataraia akikabidhi bendera kwa Viongozi wa CCM eneo la Stend  Kuu ya mabasi yaendayo mikoani na ndani ya mkoa.
Msafara ukiendelea..
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera Ndugu Happiness Runyogote katika picha na Ndugu Fahami Matsawili Mjumbe wa baraza kuu Uvccm Taifa.
Mjasiriamali wa Senene akitoa hoja zake kwa Viongozi wa UVCCM waliofika kuzungumza nao kwa lengo la kupokea changamoto zinawakabili.
 Operesheni ya Simika Bendera za CCM ikiendelea
Mazungumzo na Vijana wa Kijiwe cha Mafumbo yakiendelea
Tunaamini idadi kubwa ya wapiga kura 2020 ni vijana na sisi ni viongozi wa vijana tuna jukumu kubwa la kuwafikia vijana popote pale walipo maana kutokana na shughuli zao za kiuchumi ni vigumu kukutana nao kwa pamoja sehemu moja hivyo tumeamua kuwafuata huko huko site walipo ili tuzungumze nao Vijana wenzetu wamesema 'Viongozi wa UVCCM Taifa'
"Siasa ni Maisha ya Watu Siasa ni Watu Pia", Uvccm Mkoa wa Kagera katika harakati za kuwafikia Vijana popote walipo kwa lengo la kuzungumza nao.
Vijana Manispaa Bukoba wametakiwa kuacha kukaa vijiweni na badala yake wachangamkie fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri,Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith ametoa rai hiyo wakati akikabidhi bendera katika Vijiwe mbalimbali na kuzungumza na Vijana Mjini Bukoba.
 Ndugu JoanFaith amesema ,Vijana wanatabia ya kushinda Vijiweni na kuanza kuitupia lawama serikali kuwa haitoi ajira na kuacha fursa mbalimbali zinazotolewa zikiwemo za mikopo,alisema kutokujitokeza kwa Vijana kunasababisha kubaki katika wimbi la umasikini.
Operesheni ya Simika Bendera za CCM ikiendelea
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joan Faith Kataraia ( @joanfaith_john ) akiwa na Ndugu Fahami Matsawili mjumbe wa baraza kuu uvccm Taifa kutoka mkoa wa kagera pamoja na Ndugu Happiness Runyogote Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Vijana CCMm Mkoa Kagera katika harakati za kuimarisha chama


Muendelezo wa matukio ya picha
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu JoanFaith Kataraia akisalimiana na Wazee wa Kijiwe cha Seneti Soko Kuu Mjini Bukoba
Bendera ikikabidhiwa kwa mjumbe wa Kijiwe cha Seneti kilichopo nje ya Soko Kuu Manispaa Bukoba ni katika ziara ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joan Faith Kataraia ( @joanfaith_john ) akiwa na Ndugu Fahami Matsawili mjumbe wa baraza kuu uvccm Taifa kutoka mkoa wa kagera pamoja na Ndugu Happiness Runyogote Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Vijana CCMm Mkoa Kagera katika harakati za kuimarisha chama na jumuia ya Uvccm Mkoa Kagera.


Next Post Previous Post
Bukobawadau