Bukobawadau

NATAMANI KUONA MWALIMU WA KAGERA ANASTAAFU AKIWA TAJIRI BENKI KUNA FEDHA ZINASUBIRI MAANDIKO YENU YA MIRADI – RC GAGUTI

Na: Sylvester Raphael
Kama kuna mtumishi yeyote awe hapa au nje ya hapa tena ambaye ni mwalimu hajishughulishi kukopa kwenye taasisi za kifedha huyo anaishi tu hawezi kupata maendeleo kamwe bali atabakia kubadili mboga kila siku na kuvaa suti au kubadilisha mavazi mpaka anastaafu katika utumishi wake wa uma.
Maneno hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Septemba 23, 2019 wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB Bukoba katika siku ya walimu kwenye ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba 
Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaeleza walimu hao ambao ni wadau wakuu wa Benki ya NMB kuwa wanayo kila haki ya kufurahia maisha yao kwani Serikali inawajali lakini pia Benki ya NMB imeboresha maisha yao kupitia mikopo ambayo inawafanya wafanye kazi zao kwa uhakika na umairi mkubwa.
Mhe. Gaguti alisema kuwa mkoa wa Kagera umekuwa ukifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya kitaifa lakini sababu kubwa ni kuwa walimu wanafanya kazi yao kwa kuridhika ikiwa ni pamoja na Serikali kuwajali kwa kuwalipa mishahara na stahiki zao lakini pia Benki ya NMB imewafanya waboreshe maisha yao kwa mikopo.
“Nikiwaangalia hapa naziona nyuso za matumaini zenye bashasha na furaha lakini niwaeleze ukweli ni kwamba hata mimi baba na mama walikuwa walimu na tayari wamestaafu, kwa maisha ya sasa ya fursa zilizopo walimu waliostaafu wanatamani sana kurudi kazini kwani zamani fursa hizi za sasa hazikuwepo na sababu nyingine ni Benki ya NMB nayo imechangia sana kuboresha maisha yao”. Alisisitiza Mhe. Gaguti.
Mkuu wa Mkoa Gaguti alito rai kwa benki ya NMB kuona namna ya kuwapunguzia riba walimu sababu ni wadau wakubwa wa benki hiyo tangu mwanzo. Pia aiwataka walimu kutanua wigo wa kuunda vikundi vya pamoja mafano kwenye Kata na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu.
Naye Bw. Omari Mtiga Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi akieleza dhumuni la kukutana na walimu hao alisema kuwa ni kuwaelimisha juu ya huduma zao mpya ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao juu ya huduma za Benki ya NMB wakiwa kama wadau wakubwa wa benki hiyo. Aidha, Bw. Mtiga alisema kuwa walimu wameanzia mbali na Benki ya NMB enzi za kufanya kazi kwa makaratsi hadi sasa enzi za digitali bado ni wateja wao wakubwa.
Mwalimu Thomas Ngirwa Mkuu wa shule ya Sekondari Bukara kwaniaba ya walimu wenzake alisema kuwa Benki ya NMB ni mkombozi kwa walimu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kwani alisema kuwa shule yake ya Bukara imewahi kupata msaada wa madawati sitini kwa ajili ya wanafunzi ikiwa naye binafsi amekuwa akikopa fedha kutoka NMB kwaajili ya kusomesha watoto wake.
Mwisho, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa walimu hao kuwa mabalozi wazuri wa kulipa kodi kwa kuwa mkoa wa Kagera bado haufanyi vizuri katika kodi ambazo zinajenga miradi ya maendeleo kwa wananchi. “Popote mtakaposimama au kupata nafasi toeni elimu kwa kila mwananchi kununua bidhaa adai risiti na kuwahamasisha wanaouza kutoa risisti, walimu mna nguvu kubwa katika jamii”. Alihitimisha Mhe. Gaguti
Next Post Previous Post
Bukobawadau