Bukobawadau

MAJALIWA AKAGUA MAANDALIZI YA KUAGWA MWILI WA MZEE MKAPA UWANJA WA UHUR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi  ( wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (kushoto) wakati walipokagua Maandalizi ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam  Julai 25, 2020 ambapo  kutafanyika Ibada ya kumwombea marehemu na  kuaga mwili kitaifa kuanzia kesho. Wa nne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar, Mohammed Abood na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu , Benjamin William Mkapa wakati alipokagua maandalizi ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam  Julai 25, 2020 ambapo  kutafanyika Ibada ya kumwombea marehemu na  kuaga mwili kitaifa kuanzia kesho. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Next Post Previous Post
Bukobawadau