Bukobawadau

WATANZANIA TUNATAKIWA KUPENDANA

Adeladius  Makwega

DODOMA.

Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu, Jimbo Katoliki la Dodoma, Paul Mapalala amewataka Watanzania kupendana na kusaidiana na siyo kuwaacha wengine ili kila mmoja wetu aweze kurithi ufalme wa Mungu.

Padre Mapalala amesema hayo katika Misa ya Jumapili ya Dominika ya Januari 30, 2022 katika mahubiri yake aliyoyatoa mara baada ya masomo ya misa hiyo iliyoongozwa nayeye.

“Kweli tunataka kuupata ufalme wa Mungu lakini tunafundishwa kuwatendea wengine kama tunavyopenda siye kutendewa, je tunafanya hivyo? Huo ni wajibu wetu kufanya hivyo ili tuweze kuupata ufalme huo wa Mungu kwa pamoja. Kama wewe unautaka na mwezako pia. Watanzania tunatakiwa kupendana.”

Padre Mapalala aliongeza kuwa wakristo wanatakiwa kuwa mfano bora katika hilo kwa kualikana kuupata ufalme huo. Siyo kusema aaah yule wala, ni wajibu wetu kumshirikisha kila mmoja wetu katika ufalme huu wa Mungu, hata huyo tunayesema yule hapana.

“Kupendana ni wajibu wetu na si vinginevyo.” Aliongeza Paroko huyo wa Parokia ya Chamwino Ikulu.

Aliongeza kuwa kupenda ni jambo hili linalotakiwa kuonekana hata katika maisha ya kawaida ya kila mmoja wetu tangu katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jumuiya na jamii inayomzunguka mtu huyo.

Misa hiyo imefanyika huku hali ya hewa ya Chamwino Ikulu tangu alfajiri ya siku hii haikujaliwa kuwa na mvua, japokuwa siku kadhaa zilizopita Chamwino Ikulu ilipata neema ya mvua nyingi huku wakaazi wa eneo hilo waliopanda mazao yao yanaota.


 

Next Post Previous Post
Bukobawadau