Bukobawadau

SIMANZI KUBWA MAZISHI YA BALOZI EDWIN RUTAGERUKA

Mamia ya watu wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi uchumi wizara ya mambo ya nje Balozi Edwin Rutageruka ambaye amepumzishwa kijijini kwao Kitobo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.
Marehemu Balozi Rutageruka ameangwa Februari 19,2022 nyumbani kwao kitongoji cha Msibuka kijiji cha Kitobo wilaya ya Missenyi.
Akitoa neno kwa niaba ya familia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Dada wa marehemu Balozi Liberata Mulamula amesema kama Wizara na kama familia wamepokea kwa majonzi makubwa ya kifo cha marehemu Rutageruka ambacho kilitokea Februari 13,2022 katika Hospitali ya Aghakan Jijini Dar es salaam.
Mulamula amesema akiwa kwenye ziara ya kikazi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan nchini Ufaransa alipokea taarifa za msiba huo kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambapo baada ya kumweleza Rais taarifa hizo alimuruhusu kurudi hapa nchini kwa kwa ajili ya kuendelea na taratibu za msiba.
Katika misa takatifu iliyoongozwa na Baba Paroko wa Katoliki Parokia ya Bugango Padre Solomon Bandiho amesema kuwa, waumini wajiandalie mahusiano mazuri ya badae kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu na wamtumikie kupitia watu ambao ni wahitaji na hasa wanyonge.
"Tunapomsindikiza mwenzetu tujue utajiri tunaojikusanyia tukiwa duniani ni upendo na ukalimu kwa jamii, tukiwa duniani tumwogope Mungu na tumtumikie kupitia watu waliotuhitaji na hasa wanyonge" Amesema Padre Bandiho.
Na kuongeza kwamba, marehemu Rutageruka alijitoa kwa kanisa ambapo katika kigango cha mtakatifu Thetesia Msibuka alianzisha kampeini ya ondoa nyasi na kuhakikisha waumini wanakalia mabenchi na aliwalea vijana mijini na vijijini na kuwagharamia katika masomo.
''Kumweka Mungu Mbele kwnye kila kitu na Mungu ananiweka Mjini''
Baadhi ya Wanafamilia na Waombolezaji wakiwa wameshiriki Mazishi ya Mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka.
Viongozi wa Kiserikali wakibadilishana mawazo,Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa waKagera Meja Jenerali Charles Mbuge
Ikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao;Kwa kuwa Matendo yao yafuatana nao. Ufunio wa Yohana 14:13
Viongozi mbalimbali wakiwa wanaendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya Mpndwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka.
Muendelezo wa matukio ya picha wakati Ibada ya Mazishi  ya Mpendwa wetu Edwin Novath Rutagerukwa ikiendelea... 
Sifa kuu ya ya Omutwale Edwin Novath Rutageruka alikuwa na imani thabiti ya Kikatoliki.Alipata mascramenti ya ubatizo,komunio ya kwanza,kipaimara na ndoa takatifu
Mpendwa wetu Omutwale Balozi Edwin Rutageruka,Alikuwa mcha mungu ambaye alihudhuria Misa za kila siku asubuhi za Jumapili na alikuwa mshiriki mzuri wa Jumuia Ndogo ndogo,Na amesaidia kujenga Makanisa Dar es Salaam,Bukoba na Mwanza.
Ni Muhimu wa kutambua Mchango wa Marehemu Balozi Edwin Rutageruka wa kujenga Kigango cha Mtakatifu Theresia Msibuka-Kitobo.
Akisoma wasifu wa Baba yake mpendwa, Brayn amesema kuwa marehemu Balozi Edwin alizaliwa Oktoba 1965 katika Kijiji cha Msibuka Kata Kitobo wilayani Misenyi mkoani Kagera ameacha watoto 5  ambao ni Linda, Laura, Brayn, Cynthia na Desmond pamoja na mjane mmoja aitwaye Bi Kokuhumbya Kazaura.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akitoa Salaam za ramirambi kwa niaba ya Wizara amesema kuwa wizara hiyo itaendelea kushirikiana na familia hiyo na kuwaomba waombolezaji na wanafamilia kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Salaam za rambirambi kutoka kwa Mh.Diwani wa Kata ya Kitobo Wilaya Missenyi Ndugu Willy Mtayoba.
Salaam za rambirambi kutoka kwa mwakirishi wa TanTrade
Dr Dawson Mwema pichani kushoto akimpokea Bi Murungi Jennifer Badru Kichwabuta wakati akiwasili msibani hapo.
Balozi Edwin Rutageruka, aliyekuwa Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje pichani Enzi za Uhai wake.
Dr Dawson Mwema pichani
Taswira mbalimbali wanajamii wakiwa wamhudhuria mazishi ya Omutwale Edwin Novath Rutageruka.
Balozi Khamis Kagasheki akitoa heshima za mwisho kuaga Mwili wa Balozi Edwin Rutageruka, aliyekuwa Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje
Balozi Kagasheki mara baada ya kutoa heshima za Mwisho Mwili wa Mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka.
Mzee Pius Ngeze akitoa heshima za mwisho,Mwili wa Balozi Edwin Rutageruka
Mamia kwa mamia ya waombolezaji wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho mwili wa mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka.
Muendelezo wa matukio ya picha utaratibu wa kuaga ukiendelea...
Muendelezo wa matukio ya picha kupitia Bukobawadau...
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea...
Mjane wa Balozi Edwin Rutageruka Bi Koku akitoa heshima zake za mwisho.
Watoto wa Marehemu Balozi Edwin Rutageruka na Mjane wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao
Mzee Makubo ambaye ni rafiki mkubwa na jirani wa familia ya Balozi Rutageruka akiweka udongongo kwenye Kaburi
Balozi Edwin Rutageruka umetangulia,tutakukumbuka kwa upendo wako kwa watu,mayatima maskini na wasiojiweza hasa kijijini na vijiji jirani kwa kuweka umuhimu kwa kuwakumbuka Vijana
Dada Willielmina Balyagati na Dada Mercy pichani
Nenda Salama Balozi Edwin Novath Rutageruka
Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu Omutwale Balozi Edwin Novath Rutageruka likiingizwa kaburini.
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Prof. Faustine Kamuzora akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine
Mama Mutiganzi pichani kushoto akiwa ameungana na waombolezaji wengine katika Mazishi ya mpendwa Balozi Edwin Rutagruka
Muonekano wa Kaburi la Balozi Edwin Rutageruka,Tunamuombea pumziko la Amani
Wawata wakiweka shada la maua
...Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda...
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea kwa kuzingatia Makundi Mbalimbali
Mapadre wakiweka mashada ya maua...
Baba Askofu Kilaini akiweka Shada la Maua.
...Baba Askofu Methodius Kilaini,Askofu Msaidizi wa Jimbo katolili la Bukoba akiweka Msalaba katika Kaburi la Mpendwa wetu Balozi Edwin Rutageruka.
Ndugu Smart Baitani alifika kuhani  Msiba wa Balozi Edwin Rutageruka aliyekuwa Mkurugenzi wa Diplomasia ya uchumi Wizara ya mambo ya nje aliyepumzishwa Nyumbani kwao Kijijini Kitobo Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Ndugu Smart Baitani na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula wakiomba katika kaburi la Mpendwa wetu Balozi Edwin Rutageruka.
Muendelezo wa matukio ya picha
Wanafamilia na Wanaukoo katika picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu kabla na baada ya mazishi ya Mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka.
Bi Koku Mjane wa Balozi Edwin Rutageruka na Watoto wake katika picha ya kumbukumbu
Familia ya Mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka katika picha ya pamoja kwa ajiri ya kumbukumbu.
Wanafamilia katika picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu kabla na baada ya mazishi ya Mpendwa wetu Balozi Edwin Novath Rutageruka
Alhaji Chuchu pichani
Viongozi wa Serikali ya Mkoa Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge mapema wakiwasili msibani hapo kijijini Kitobo Wilaya ya Missenyi.
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote pale wasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045










 

Next Post Previous Post
Bukobawadau