Bukobawadau

YALIYOJILI KATIKA KIKAO CHA POSTA MKOA KAGERA AGUST 20,2022

Meneja wa Mkoa wa Kagera wa Shirika la Posta Ndugu Joseph Mutatina pichani akizungumza  katika Kikao kilihudhuriwa na Wafanyakazi wote wa Posta Bukoba na Posta Masta wa Wilaya zote za Mkoa Kagera na Wilaya ya Chato kilichofanyika tarehe 20/08/2022 katika ukumbi wa Bukoba Coop.Mgeni Mwalikwa katika kikao hicho  alikuwa Mkufunzi wa Chuo cha Zoom Politytechinic College Ndugu Gidion Leonard Gwima aliweza kutoa  somo kuhusu huduma kwa Wateja.

Ndugu Patrick Mwakajeli Mhasibu wa Posta Bukoba akifatilia jambo kupitia simu yake ya kiganjani
Mkufunzi wa Chuo cha Zoom Politytechinic College Ndugu Gidion Leonard Gwima akitoa somo la huduma kwa wateja katika kikao cha Wafanyakazi wa Posta Kagera.

Mwezeshaji akiendelea kutoa somo la huduma kwa wateja katika kikao hicho.
Muendelezo wa matukio ya Picha kikao kikiwa kinaendelea..
Wafanyakazi wakiendelea kufuatia mada mbalimbali zinazoendelea
Wafanyakazi wa Posta walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kimkakati.
Katika kikao hicho imeelezwa kuwa
Mpango mkakati wa 7 (2019/20-2023/24) umesitishwa ili kukidhi mahitaji ya soko na kuendana na mikakati na agenda za kitaifa na kimataifa.(refer leaflet)
Mwenyekiti wa Kikao hicho  Meneja wa Mkoa wa Kagera wa Shirika la Posta Ndugu Joseph Mutatina akitoa mrejesho wa kikao cha management ya Shirika la Posta kilichofanyika Mkoani Morogoro tarehe 5/8/2022 na kujadili kwa pamoja mikakati ya kuongeza mapato ya Posta Kagera.

 MIKAKATI YA KUONGEZA MAPATO
2.1 Kufungua Posta Rubya iliyokuwa imefungwa zaidi ya miaka 3. Hii imeonekana kuwa na fursa nyingi hivyo kuwa na mategemeo ya kupata biashara. Rubya kuna Taasisi nyingi ambapo tukifungua Posta tutapata biashara. Kwa kuanzia kupunguza gharama tutatumia intern ila baadae tutaomba staff mwenye PF ili tufanye na biashara ya uwakala wa benk.

2.2 Kutoa huduma za uwakala wa aina zote (m.pesa, tigopesa, halopesa, airtel money,T.pesa) kwenye duka la Posta HPO

2.3 Kuuza vocha zote za simu i.e Vodacom, TTCL, Tigo, airtel
2.4 kutafuta mpangaji kwenye jingo lililo wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 168. Pia tunatafuta mpangaji ambaye anaweza kulikarabati mwenyewe na kutukata kwenye kodi.

2.5 Kuboresha internet café kwa kuweka usiri wa wateja na kuongeza vitendea kazi kama camera (kwa ajili ya picha za passport size), scanner, lamination machine na printer ya rangi
2.6 Kuhamasisha Taasisi zinazoaminika kusaini mkataba wa kununua ticket za ndege ya ATCL kwa mkopo. Kulipa kwa mkopo (billing) itasaidia kuwashawishi wateja kutumia huduma zetu.

2.7 Kuzuia Taasisi mbili au zaidi kutumia Sanduku la Barua moja. Mfano unakuta Shule kadhaa zinatumia Sanduku la Mkurugenzi. Hii tutaifanya kupitia kwa (a) Mwanasheria wa Shirika kututafutia kipengere cha sheria kinachotaka kila Taasisi kuwa na anwani yake iliyosajiliwa. Na baada ya hapo ni kuwaandikia wateja muda wa mwisho wa kushea Sanduku la barua.(b) kupitia TRA (c) KUpitia kwa wakurugenzi wa Halmashauri

2.8 Kutembelea wateja wa EMS wengi inavyowezekana na kuwashawishi kutumia huduma zetu zilizoboreshwa baada ya kurudisha usafiri wa barua kwa ndege. (list ya wateja walipotea)
2.9 Kuzungukia maduka mengi inavyowezekana kusajili maduka kwenye duka letu la Posta Mtandao. (doc/manual to be sent)
Kuboresha usafiri ngara next week majibu

2.10 Kupitia kwa Wakuu wa Shule, kuhamasisha somo la uandishi wa barua na kuwapa wanafunzi zoezi/mtihani wa uandishi wa barua. Zoezi hili litaenda sambamba kufungua vituo vya kuuza stemp mashuleni.
2.11 Kuwatafuta na kuwashawishi wafanyabiashara wa mazao ya ziwani wanaouza mazao yao nje ya nchi kupitisha Posta
2.12 Kutumia ipasavyo mfumo wa anwani za makazi na postcode.
2.13 Matumizi makubwa ya kidigitali ambayo yatahusisha kuimarisha mfumo wa pmis, mafunzo ya IT, nk
2.14 Kuimarisha kitengo cha customer service na kuimarisha track and trace, kuimarisha ulinzi wa mizigo ya wateja, kujisajili ISO na kuongeza vitendea kazi.
2.15 Kutoa mtaji wa biashara ya posta cash
2.16 Kushirikiana na wadau kuimarisha huduma Pamoja.
2.17 Kuwa na kitengo cha logistics
2.18 Kuanzisha kitengo cha cost accounting
2.19 Kuongeza matangazo ya Shirika (Brand awareness)
Ndugu Justin Katemelo pichani akitoa mchango wake wa mawazo katika kikao hicho
Wafanyakazi wa Shirika la Posta  Mkoa Kagera wakiendelea kuchangia mada mbalimbali.
Mafanikio ya Mkoa
• Kupunguza gharama kwa kusitisha kupeleka sampuli Maabara kuu na kuanza kupeleka Hospitali ya Bugando
• Kuongezeka maduka mtandao
• Kutundika mabango ya kutambulisha Ofisi yay a Bukoba na Biharamulo
• Kusafirisha barua/vifurushi vya EMS kwa njia ya ndege kila siku
• Kukusanya ada ya masanduku ya masanduku yote na kuongeza masanduku mapya 100 (Muleba)
Matukio ya picha wakati kikao kikiendelea
Muendelezo wa matukio ya picha.

Wafanyakazi wote wa Posta Bukoba na Posta Masta wa Wilaya zote za Mkoa Kagera na Wilaya ya Chato wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Mwalikwa
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu
 

Mafanikio ya Mkoa
• Kupunguza gharama kwa kusitisha kupeleka sampuli Maabara kuu na kuanza kupeleka Hospitali ya Bugando
• Kuongezeka maduka mtandao
• Kutundika mabango ya kutambulisha Ofisi yay a Bukoba na Biharamulo
• Kusafirisha barua/vifurushi vya EMS kwa njia ya ndege kila siku
• Kukusanya ada ya masanduku ya masanduku yote na kuongeza masanduku mapya 100 (Muleba) 

Next Post Previous Post
Bukobawadau