Bukobawadau

POSTA KAGERA WAADHIMISHA SIKU YA POSTA DUNIANI LEO OCT 9,2022

Katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani, Shirika la Posta Kagera  leo tarehe 9 Oktoba 2022 wamezungumza na wanahabari na kuwaeleza wananchi kupitia 88.5 Kasibante FM  kuhusu huduma za Posta pia wametembelea  kituo cha Watoto cha Ntoma Orphanage kilichopo Maruku
Katika kuadhimisha siku ya Posta duniani leo tarehe 9/10/2022, Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta, Mkoa wa Kagera Ndugu Joseph Mutatina pichani kushoto amekatana na waandishi wa habari wa Kasibante FM Radio na kuelezea huduma zitolewazo na shirika la Posta kama 
1.Usafirishaji kwa njia ya haraka
- huduma ya ems,kusafirisha kifurushi kwa ems, kusafirisha sampuli za maabara
2 Usafirishaji kw anjia ya kawaida
-Kusafirisha barua kwa kawaida ,kwa regista ,kusafirisha vifurushi ,posta mlangoni ,Postacarg
Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta, Mkoa wa Kagera Ndugu Joseph Mutatina ameelezea namna wanavyoadhimisha siku ya Posta duniani. Ameeleza matukio ya Posta mwaka huu kuwa ni pamoja na mashindano ya uandishi wa barua kwa wanafunzi, isha kwa makundi mbalimbali, makala kwa wanahabari, ubunifu wa graphics na tehama. Katika mashindano hayo Meneja wa Mkoa ndugu Joseph Mutatina amebainisha kuwa Mkoa wa Kagera umefanikiwa kupata mshindi wa tatu katika mashindano ya uandishi wa Barua. Ametaja kuwa mshindi wa tatu ametokea kashai sec na kutaja jina la mshindi kuwa ni Warida Mohamed. Ametoa pongezi nyingi kwa mshindi na Mkuu wa Shule Kashai Mwl Lydia. Ametaja kuwa mshindi hadi anaongea na waandishi wa habari yuko Dar ambako siku ya Posta inaadhimishwa kupokea zawadi yake atakayokabidhiwa na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.
Pia ametaja kuwa katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi wa Posta ofisi ya Bukoba wataenda kutoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha Ntoma Orphanage.

Meneja wa Mkoa ndugu Joseph Mutatina amebainisha kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni 'Posta kwa kila mtu'. Alitaja Posta kwa kila mtu maana yake inajihusisha na maeneo mbalimbali kama  Afya hapa wanashirikia na Wizara ya Afya kwa kusafirisha  sampuli za maabara  kote nchini kutoka kwenye vituo vya Afya ,Usalama wa Taifa, Ukaribu wa  Wizara ya viwanda na biiashara,Shirika la posta wanashirikiana na Baraza la mtihani (NECTA) na bodi ya mikopo katika kuwasaidia wanafunzi kufanya Usajiri.
Maeneo mengine ni Eneo la Uchumi,Usafirishaji,Utoaji wa huduma mbalimbali za Serikali kwa Wananchi,Eneo la Utalii katika kutangaza vivutio vya Tanzania kupitia uchapishaji wa stempu na eneo la tehema ambapo huduma zao zinapatikana  kidijitali.
Wafanyakazi wa Posta Ofisi ya Bukoba walipotembelea na kutoa  msaada kwenye kituo cha watoto Watoto cha Ntoma Orphanage.
Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta, Mkoa wa Kagera Ndugu Joseph Mutatina akimkabidhi zawadi ya Keki msimamizi wa Kituo cha watoto cha Ntoma Orphanage
Msimamizi wa kituo cha Ntoma Orphanage akimlisha Keki Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta, Mkoa wa Kagera Ndugu Joseph Mutatina
Utaratibu wa keki ukiendelea 
Zawadi kutoka kwa Wafanyakazi wa Posta Ofisi ya Bukoba
Wafanyakazi wa Posta Ofisi ya Bukoba wakipata ufafanuzi na historia fupi ya kituo hicho kutoka kwa msimazi wa kituo
Picha mbalimbali Wafanyakazi wa Posta Ofisi ya Bukoba katika maashimisho ya Siku ya Posta Duniani
Sehemu ya Jengo la kituo cha Watoto cha   Ntoma Orphanage
Picha mbalimbali Wafanyakazi wa Posta Ofisi ya Bukoba katika maashimisho ya Siku ya Posta Duniani







 

Next Post Previous Post
Bukobawadau