Bukobawadau

SERIKALI YAWATOA HOFU WAFANYABISHARA

Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka (katikati), akimsikiliza Mhandisi kutoka Shirika la Reli Nchini (TRC), Mkoa wa Tanga Patience Karumuna, kuhusu hatua ya ukarabati iliyofikiwa wakati Mkurugenzi huyo alipokagua maendeleo ya kazi hiyo Mkoani Tanga.

Sehemu ya Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Sekta Binafsi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao cha Wadau cha Maboresho ya Bandari ya Tanga (Tanga Port Improvement Committee), Mhandisi Aron Kisaka (hayupo pichani), wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika hivi karibuni jijini  Tanga

Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga, Mhandisi Masoud Mrisha (mwenye Kaunda suti nyeusi), wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa reli inayoingia Bandari ya Tanga jijini humo hivi karibuni.

Kichwa cha treni chenye namba 8801-TRL kikifanya majaribio kwenye njia ya relu kuingia katika Bandari ya Tanga.

Picha na WUU

SERIKALI YAWATOA HOFU WAFANYABISHARA

Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuwa itaendelea kuboresha miundombinu na mifumo ya usafirishaji ili kurahisisha shughuli za usafiri na usarishaji wa abiria na mizigo baina ya mikoa hiyo na nchi jirani.

Akizungumza jjini Tanga mara baada ya ukaguzi wa maboresho ya reli inayoingia bandari ya Tanga Mkurugenzi wa Huduma za Huduma za Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga, Mhandisi Aron Kisaka, amesema kukamilika kwa ukarabati na kukabidhiwa kwa sehemu ya gati lenye mita 300 lazima uende sambamba na maboresho ya miundombinu mingine ili kurahisisha utoaji wa mizigo bandarini.

“Kama wataalam tunazingatia sana utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yote hatuwezi kuboresha bandari hii tukaacha kutizama miundombinu saidizi iko kwenye hali gani, kwa hatua hii iliyofikiwa matokeo yameanza kuonekana ambapo ongezeko la mizigo kwa mwezi Septemba kwenda Oktoba limefika asilimia 41%,” alisisitiza Mha. Kisaka

Mhandisi Kisaka amesema lengo la Bandari ni kuhakikisha mzigo unaingia na kutoka kwa haraka ili kuongeza ufanisi na kuongeza zaidi shehena ya mzigo unaohudumiwa na bandari hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Tanga, Mhandisi Masoud Mrisha, amesema utekelezaji wa mradi wa maboresho ya bandari hususani gati mbili 

unasimamiwa kwa karibu na unatarajiwa kukamilika mwezi aprili mwakani.

Mha. Mrisha ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi pamoja na miundombinu mingine bandarini hapo kutawezesha zaidi ya tani zaidi ya milioni mbili kwa mwaka na kutasababisha kushuka kwa bei za bidhaa mbalimbali sokoni.

Naye Mhandisi Patience Karumuna (wa kwanza kulia) kutoka Shirika la Reli Nchini (TRC) amesema kazi ya ukarabati wa reli kutoka stesheni ya Tanga mpaka bandarini ilikuwa umeshakamilka na kichwa cha treni kufanya majaribio lengo likiwa kubaini mapungufu yaliyobaki baada ya ukarabati.

(Imetolewa na kitengo cha habari na mawasiliano Serikalini Wizara ya ujenzi na uchukuzi) 

Next Post Previous Post
Bukobawadau