Bukobawadau

KATIKA PICHA MAPOKEZI YA MWILI WA BALOZI DR KAMALA

Ni Simanzi kubwa mapokezi ya Mwili wa Balozi Kamala
Jeneza lenye Mwili wa  mpendwa wetu
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Erasto Siima amewaongoza wananchi katika Mapokezi ya Mwili Wa Balozi Dr.Kamala Katika Uwanja wa Ndege Bukoba mapema ya Leo Jumapili Feb 18,2024
Balozi Dr Kamala aliwahi kuwa Waziri wa Afrika Mashariki na Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoa wa Kagera kuanzia mwaka 2000 hadi 2010, mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri Kamili mwaka 2008 hadi 2010
Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.
Mashishi yake yanatalajiwa kufanyika Siku ya Jumanne Feb 20,2024Nyumbani Kwake Kijijini Bwanjai-Mugana Wilayani Missenyi
Picha na Mc Baraka *
Msafara kuelekea Hospital Kuu ya Mkoa Kagera Utakapohifadhiwa Mwili wa Balozi Dr.Kamala

Next Post Previous Post
Bukobawadau