Bukobawadau

MAWAZIRI WATATU WAJADILI MAENDELEO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb), wamekutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya Sekta ya madini na uwekezaji ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na wajumbe wengine kutoka Wizara hizo tatu

 

Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb), akieleza kuhusu maendeleo ya sekta ya madini wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) (hawapo pichani), uliofanyika Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akieleza kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya madini katika kukuza Uchumi wakati wa mkutano wake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) (katikati) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb), kushoto, uliofanyika Treasury Square, jijini Dodoma.


 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb) (hawapo pichani), jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, akieleza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb) (hawapo pichani), uliofanyika Treasury Square, jijini Dodoma.

Next Post Previous Post
Bukobawadau