🎉Maadhimisho Miaka 15 ya Josiah Girls’ Secondary School 🌟
Katika kuadhimisha miaka 15 ya mafanikio, sherehe imehusisha Ibada Kuu ya Shukrani iliyoongozwa na viongozi wa dini, serikali na jamii.
🔹 Askofu Dkt. Alex Malasusa (KKKT) alisisitiza uongozi wa Mungu katika safari ya shule.
🔹 Askofu mstaafu Methodius Kilaini alipongeza mshikamano na uthubutu wa uongozi wa shule.
🔹 Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara alitambua mafanikio makubwa ya kitaaluma.
🔹 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Erasto Siima, aliahidi ushirikiano wa serikali kuboresha miundombinu na elimu.
Shule imeendelea kushirikiana na wadau wa elimu, wazazi, na jamii huku ikikuza vipaji, maadili, na kuhamasisha matumizi ya teknolojia na AI kwa kizazi kipya.
Kutoka kushoto pichani ni Mjumbe wa Bodi ya Shule na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Dkt. Abednego Keshomshahara,Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa na Askofu mstaafu wa jimbo Catholic la Bukoba Ask. Methodius Kilaini wakipanda Mti kwa pamoja kama ishara ya kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa shule ya Josiah Girls.
Shule ya Sekondari ya Wasichana Josiah imeadhimisha Miaka 15 tangu kuanzishwa kwake kwa Ibada Kuu ya Shukrani iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa.
Katika mahubiri yake, Askofu Malasusa alisisitiza kuwa “Mungu hayuko mbali na shule hiyo na atawasimamia na kuhakikisha wanashinda kwa kuwa Yeye amejaa neema. Hata sasa Bwana amesaidia.....
🎥 BukobaWadauLive 🎥📍 Habari | Michezo | Burudani | Maarifa
✨ Usikose Updates Kila Siku!
👍 Subscribe & Share ili kuunga mkono kazi yetu na kuendelea kupata taarifa muhimu.
🌐 Jiunge na jamii yetu na uwe sehemu ya mazungumz0
LINK YA YOUTUBE BUKOBAWADAULIVE
Shule ya Josiah, iliyoanzishwa mwaka 2010 katika Kata ya Ijuganyundo, Manispaa ya Bukoba, imekuwa kimbilio kwa wazazi na walezi kutokana na elimu bora na malezi yenye maadili.
Mjumbe wa Bodi ya Shule na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Dkt. Abednego Keshomshahara, alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa tangu kuanzishwa kwake.
Maadhimisho haya pia yalihusisha utoaji wa tuzo kwa wadau waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya shule pamoja na shuhuda za wanafunzi na wahitimu.
Kwa jumuiya ya Josiah Girls Secondary School, miaka 15 ni ishara ya baraka, mshikamano na matumaini ya mafanikio makubwa zaidi katika siku zijazo.




.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
DFGH.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
sdfghn.jpg)
