UCHUMI WA TANZANIA UMEKUA KWA 5.4 ROBO MWAKA YA KWANZA 2025
Na. Joseph Mahumi, WF, Dodoma
Akizungumza Bw. Blancher, katika taarifa iliyochapishwa
katika tovuti rasmi ya Shirika hilo, alisema kuwa baada ya ziara yao,
wameona uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa thabiti, ambapo umekua kwa
asilimia 5.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025 (kuanzia Julai hadi
Septemba), huku mfumuko wa bei ukibaki katika kiwango cha chini cha
asilimia 3.4 mwezi Agosti. Sekta za madini, kilimo, viwanda na ujenzi
ndizo zimekuwa nguzo kuu za ukuaji huo.
IMF ilibainisha kuwa
matarajio Chanya ikiwemo mageuzi ya mapato kupitia Mkakati wa Muda wa
Kati wa Mapato (Medium-Term Revenue Strategy) yanatarajiwa kuongeza
ukusanyaji wa mapato na kuwezesha uwekezaji zaidi katika sekta za
kijamii.
Aidha, aliongeza kuwa uboreshaji wa soko la fedha za kigeni umeongeza ukwasi na kupunguza tofauti kati ya soko rasmi na lisilo rasmi.
Nakisi ya akaunti ya sasa imeshuka hadi asilimia 2.5 ya Pato la Taifa katika mwaka wa fedha 2024/25, ikichangiwa na mauzo ya madini, bidhaa za kilimo na utalii. Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 6.2 kufikia Julai 2025, sawa na miezi minne ya uagizaji bidhaa.
IMF inatoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania, washirika wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia kwa ukarimu na majadiliano yenye mafanikio wakati wa ziara hiyo.




