Bukobawadau

Mwelekeo Mpya Missenyi: Uchaguzi Waamua Viongozi Wapya Halmashauri

Taarifa Rasmi Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi umekamilika leo katika ukumbi mdogo wa Halmashauri, ambapo jumla ya Madiwani 27 pamoja na Mbunge wa Jimbo la Missenyi walihudhuria na kushiriki zoezi la kupiga kura.

Matokeo ya Uchaguzi wa Mwenyekiti

Zoezi la kuhesabu kura lilionesha ushindani mkubwa kati ya wagombea watatu waliochuana kwenye nafasi ya Mwenyekiti.
Matokeo ni kama yafuatayo:

Phocus Rwegasira – kura 16

Jamary Suleiman Rulengwa – kura 10

Regina Rwamuganga – kura 2


Kwa ushindi huo, Phocus Rwegasira ametangazwa kuwa jina lililopendekezwa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kama Mwenyekiti.

Matokeo ya Makamu Mwenyekiti

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ushindani ulikuwa mkali pia, ambapo matokeo yalikuwa:

Kiiza Joshua – kura 15

Domisian Nshekanabo Nshambya – kura 13

Lydia Hima – kura 8

Kutokana na matokeo haya, Kiiza Joshua ameibuka mshindi na kuwa  kinara wa nafasi ya Makamu 
#BukobawadauMedia#MissenyiUpdates#Missenyi
#UchaguziWaViongozi
#BukobawadauReflections

 @Bukobawadau BukobawadauLIVE
 

Next Post Previous Post
Bukobawadau