SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

02 March 2014

VITUKO VYA WANANCHI BAADA YA GARI LA BIA KUANGUKA MAENEO YA KEMONDO JIONI YA LEO MARCHI 1,2014

Ni ajali  iliyotokea jioni ya leo Jumamosi marchi 1,2014 majira ya ya saa kumi alasiri ambapo gari gari aina ya Semi Trela mali ya kampuni ya Zachwa Investment ya Mjini Bukoba   lililokuwalimesheheni sanduku za chupa za bia zenye vileo kuanguka katika kijiji cha Kemondo.
Wanakijiji walivamia gari hilo baada ya kugundua nini kilichomo
 Hakuna kifo kilichotokea  baada ya gari lililokuwa limebeba sanduku za bia zenye pombe kuanguka.
Licha ya kontaina  la gari kuwa limefungwa bado wananchi walifanya mikakati yao kwa kuchimba Shimo ili  maji ya bia yaweze kuingia .
 Baada ya hapo ikawa kama sherehe kwa wanakijiji 
 Wakazi wa Kijiji cha kemondo wakipata kinywaji cha bwelele.
Hiki ndicho kilichotokea baada ya Gari la bia kuanguka na wanakijiji kukusanyika na kushambulia  kinywaji kilichokuwa kinatiririka  kufuatia kupasuka kwa chupa za bia katika ajali hiyo.

6 comment:

Anonymous said...

Yaani nimesikitika kuona hizo picha, sio sababu ya bia bali sababu ya hao watu wanaochota bia kunywa.

Angalia kwanza hawafikiriii afya zao bali wanafikiria BURE. Haya kutu, vipande vya chupa vidogo vidogo visivyoonekana, etc

Wao wanakunywa tuuuu, kweli tunahitaji sana kuelimishana, kweli katika watu wote hapo hakuna aliyejua kuwa kuna madhara? Na polisi huko hawapo? Je na likisogea na kujiroll tena hawafikirii hili(naona wanadokoa kutoka upande na shimo wakachimba) inasikitisha.

Jamani wahaya inabidi kusaidiana na kuelimishana sana.

Anonymous said...

Inasikitisha sana

Anonymous said...

Duh bukoba tambarale

Anonymous said...

Kweli bado tuna safari ndefu!!

Anonymous said...

Huu si ulevi ni urafi usio na maana! watu wazima tunafanya mambo ya kijinga!! haiwezekani watu wote walokusanyika pale kwamba walishindwa kukemea tabia hiyo! mmetutia aibu mkome kupenda vya bure.

Anonymous said...

Hatari elimu inahitajika

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU