Bukobawadau

MWANA WA MFALME WILLIAM HATIMAE APATA MKE


Mwana wa mfalme wa uingereza,Prince William na Kate Middleton
wamefunga ndoa katika kanisa la Westminste Abbey jijini London.
Takribani wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa
na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.

Maharusi hao walishangiliwa na maelifu ya watu waliojipanga barabarani
kuelekea kasri ya Buckingam Palace ambako malkia amewaandalia karamu
wageni 650.

Wana ndoa hao walitumia gari lililovutwa na farasi la muundo wa mwaka
1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka1981.
Baadaya kulishana viapo vya ndoa,Askofu mkuu wa Canterbury,Rowan Williams.
Aliwanadi rasmi "mume na mke"kwamba kuanzia sasa maharusi hawa watajuloka
na rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge.
Next Post Previous Post
Bukobawadau