Bukobawadau

Bin Laden 'alipanga shambulizi jipya'

Nyaraka zilizopatikana katika nyumba ya Osama Bin Laden zinaonyesha kuwa alikuwa na mipango ya kuishambulia tena Marekani ikiwemo wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya Septemba 11, taarifa kutoka Marekani zimearifu.
Usafiri wa reli.

Mpango mmoja ulilenga kushambulia usafiri wa reli Marekani, ripoti zinasema, ingawa hakukuwa na taarifa za tishio la moja kwa moja lililogunduliwa.

Maafisa wanachunguza kompyuta, DVDs na nyaraka nyingine zilizochukuliwa kutoka kwenye nyumba hiyo Abbottabad ambako wanaamini Bin Laden alijificha kwa miaka sita.

Rais Obama anatarajia kukutana na baadhi ya vikosi vilivyohusika katika operesheni hiyo.

Atakuwa na mkutano wa faragha Fort Campbell, Kentucky, na baadhi ya Wanamaji walioendesha operesheni hiyo.

Alhamis, Rais Obama alizuru eneo la Ground Zero lililokumbwa na shambulio la Septemba 11 2001 mjini New York , na kuweka shada la maua ikiwa ni kumbukumbu ya karibu watu 3,000 waliothiriwa na shambulio hilo.

Aliziambia familia za waliothiriwa kuwa haki sasa imetendeka lakini Marekani 'haitasahau.'
Next Post Previous Post
Bukobawadau