Bukobawadau

Breaking newzzzzzzzz!!Ajari mbaya 16 Wapoteza maisha.

Sheraton bus baaada ya ajari.

JINAMIZI la ajali linaendelea kuikumba nchi baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika mji wa Geita mkoani Mwanza na kusababisha watu 15 kufariki papo hapo na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Ajali hiyo ambayo ilisababisha mji huo kuzizima ilitokea jana majira ya 2:40 asubuhi katika eneo la kijiji cha Chibingo kata ya Nyamigota, tarafa ya Busanda, baada ya gari la Bunda Bus lenye namba za usajili T 810 BDW kugongana na basi la Sheraton lenye namba za usajili T 268 AJC.

Mashuhuda wa ajali hiyo waliiambia bukobawadau blogspot kuwa gari la Bunda Bus lilikuwa likitokea jijini Mwanza kwenda wilayani Karagwe mkoani Kagera, huku basi la Sheraton likitokea wilayani Bukombe mkoani Shinyanga kwenda jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa habari hizo, chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa mabasi yote mawili, na kwamba wakati ajali hiyo ikitokea basi la Sheraton lilikuwa likijaribu kulipita gari fuso leenye namba za usajili T 823 BPU, kisha kugongana uso kwa uso na basi hilo jingine
.
Ajari mbaya ya bus la Sheraton baada ya kugongana na bunda bus.
Bunda bus express iliyokuwa ikisafiri kutokea Mwanza kuja Bukoba mjini na kuelekea Karagwe baada ya ajari.
Mabaki ya viti Bunda bus ambapo watu sita wamekufa papo hapo.Imeripotiwa mpaka sasa watu 16 wamepoteza maisha.(wadau tuwaombee wenzetu waliotangulia mbele ya haki, amen!
Next Post Previous Post
Bukobawadau