Bukobawadau

Kinga ya kuzuia kuenea Ukimwi

Utafiti uliofanywa pamoja na majaribio katika kinga mpya umedhihirisha kuwa kinga hii mpya imefanikiwa kukinga tumbiri asiambukizwe virusi vinavyosababisha ukimwi na kutokana na hilo kutowa ishara kwamba kuna uwezekano mpya wa kukabili kinga ya maradhi ya ukimwi.
mtaalamu ajaribu kinga ya ukimwi

Watafiti wa huko Marekani wanasema kuwa walifanya majaribio hayo kwa kuwapa kinga tumbiri 13 kati ya 24 waliotumiwa.

Baada ya mwaka mzima baada ya majaribio hayo iligundulika kuwa kati ya Tumbiri wote hao 12 kati yao walikuwa bado wana kinga dhidi ya virusi vya ukimwi mwilini.

Matokeo hayo yaliyochapishwa katika jarida la sayansi, Nature, huenda yakawa mchango muhimu katika utengenezaji wa kinga maalum dhidi ya maradhi hatari ya ukimwi na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Wataalamu hao waliwadunga tumbiri 24 wasiokuwa na maradhi yoyote kinga iliyokuwa na mfano wa virusi uliotengenezwa katika maabara, rhesus cytomegalovirus (CMV).

Kinga hii ilitengenezwa kwa ajili ya kuunda sumu ya kushambulia ugonjwa wa ukimwi unaowakumba tumbiri (SIV) sawa na HIV kwa Binadamu.

Baada ya kipindi cha mwaka mzima ilibainika kuwa kinga hiyo ilikuwa na uwezo kamili dhidi ya ukimwi wa Tumbiri kati ya tumbiri 13 tu, ikiwa nusu ya idadi hiyo iligundulika kuwa na kinga baada ya kipindi cha mwaka mzima.

Kinga hiyo ilitumiwa kwa kushinikiza uzalishaji wa aina ya seli fulani ya damu, seli zijulikanazo kitaalamu kama "effector memory T-cells", ambazo hubaki kuwa imara mwilini kwa kipindi kirefu hata baada ya virusi kuteketezwa na kutowa ulinzi wa mwili kwa kipindi kirefu.

Kiongozi wa mradi huo Profesa Louis J Picker, wa taasisi ya tiba ya kinasaba huko Oregon, anazilinganisha seli hizi na askari imara wa kulinda doria.

"ni mfano wa askari wanaorejea kambini na kutelekeza silaha zao, kwa imani kuwa wenzao wanaendeleza kazi bila wasiwasi," Profesa Louis Picker aliambia BBC.

Aliongezea kusema kuwa kuna ushahidi kwamba kinga hiyo iliteketeza dalili zote za ukimwi (SIV) katika tumbiri wote, sababu aliyoielezea kama inayowezekana kwa ukimwi wa binadamu.

Next Post Previous Post
Bukobawadau