Bukobawadau

Bukoba yetu Jumapili hii

Ni makutano ya barabara kuu itokayo Muleba kuingia bukoba mjini na ile itokayo Kyaka kuingia bukoba MJINI.
Kumbukumbu zinaonyesha ufunguzi rasimi wa eneo hili na barabara hii,ulifanyika kipindi cha Serikali ya awamu ya tatu ambapo Rais Mkapa aliambatana na Mawaziri wake sita.Kikubwa ni hari ya utata wa eneo hili ajari za kila siku,vipimo visivyo yakinika ukarabati husio isha kila mara tokana na ubovu unaojitokeza.Inakuwa shida saana kwa wageni wetu hasa madereva kumudu eneo hili hasa wa magari makubwa, bila shaka ndg mdau wewe ni sehemu ya watu wanaotatizwa na sehemu hii hapa.Na kwa mbali kabisa kilimani ndipo ilipo shule mama,Omumwani sekondari.Ilikuwa mtu akifika eneo hili lazima anyooshe kidole kuongelea shule hiyo ambayo ndiyo ilikuwa nuru ya mkoa wetu kiujumla.lakini kwa sasa hatima yake aijulikani kabisa,na si tu kwa ubora wa tahaluma bali pia kwa ubora wa majengo hali inasikitisha kama sio kusitajabisha.


Pita pita maeneo ya Hamgembe maarufu kama kwa phocas.
>
Matengenezo ya bustani ya kisasa katikati ya mji wa bukoba unaendelea maeneo ya stendi na ujenzi wa picha ya sanamu la mgomba kama ishara ya kilimo chetu cha Ndizi.

Jengo la ofisi ya Mamlaka ya mapato (TRA)

Kama inavyo onekana katika picha,vijana wengi hutumia pikipiki kwa kujipatia kipato ili kuweza kumudu maisha ile hali na wananchi wengi pia utegemea usafiri huo maarufu kama Asecdo kutokana na unafuu wa bei.

Uwanja wa uhuru uliopo kata ya Bilele na Sanamu la Mayunga kama jemedari wa vita ya kagera

Mwonekano wa Msikiti wa Bilele ambapo ujenzi bado unaendelea

Hivi ndivyo ilivyo onekana kwenye lango la hospitali kuu ya mkoa.Mtu akichelewa (ucheza)na mlinzi ili aweze kupita.Wadau swala hili limekuwa la kawaida na wala sio tatizo tena wadau wngi wanasema hiyo sio rushwa na wala sio kikwazo kwao,wao wanarahani kitendo cha kiongozi mkubwa mwenye mammlaka kuingiza dawa feki nchini na kuzibitisha zinaubora.Baada ya mda wizara husika hutoa taarifa kwamba dawa fulani hazifai kwa afya ya binadamu,dawa fulani azitibu maralia na mambo kama hayo na hiyo ndio rushwa wadau wengi wanayo ipigia kelele (ufisadi mkubwa).
Jengo la posta lililopo mkabara na bukoba sekondari jirani kabisa na mtu maarufu mjini bukoba ajulikanae kama Mzee Mitto.
Next Post Previous Post
Bukobawadau