Bukobawadau

MTETEZI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA AUAWA

Mauaji ya kikatili ya mwanaharakati wa kutetea mapenzi ja jinsia moja kutoka Afrika kusini yamelaaniwa na kuelezwa kama uhalifu unaohusishwa na chuki na shirika la Human Rights Watch.

Shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Marekani limewasihi polisi kufanya jitihada zaidi ya kuwapata waliohusika na mauaji ya hivi karibuni na ubakaji wa Noxolo Nogwaza

Aliuliwa kwa kupopolewa na mawe na kuchomwa kisu Aprili 24 baada ya kutokea mabishano kwenye baa katika kitongoji cha KwaThema, mashariki mwa Johannesburg.

Wanaharakati wamesema wapenzi wa jinsia moja wa kike nchini humo hulengwa kwa kile walichosema "ubakaji wa kurekebishwa".

Tofauti na nchi nyingi za Afrika, mapenzi ya jinsia moja ni halali Afrika kusini na katiba inaharamisha ubaguzi kwa misingi ya jinsia yako.

Lakini wanaharakati wamesema wapenzi wa jinsia moja hushambuliwa kwenye vitongoji mbalimbali.

Polisi wamesema wanafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo na wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti.

Next Post Previous Post
Bukobawadau