Bukobawadau

Breaking newzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!Miss Kagera apatikana ni Janeth Abdul

Ile tu michuano inaanza na mamiss wakipita jukwaani kwa ufunguzi tayari hali ilikuwa ngumu kwa majaji kutokana na uwiano na vigezo kuonekana kushabihiiana kama si kulandana kwa ukaribu saana.
Miss Kagera 2011 Miss Janeth Abdul akivujwa taji mara tu baada ya kutangazwa mshindi.Na mshindi wa pili ni Denise Apondi na mshindi wa tatu ni Miss Beatrice Marwa ambae ni mshiriki aliye iwakilisha Bukoba mjini.
Mshindi wa kwanza na wapili ni wawakilishi wa wilaya ya Muleba.

Mzuka ulimpanda mtu mzima 20% wakati wa show ya kuwasindikiza warembo alimanusura jukwaa lididimie kutokana na wadau kumpokea vizuri msanii huyu nguri mwenye staili ya kuimba kwa majonzi ile hali anafurahisha.
Mgeni wa heshima RPC mkoa wa kagera Ndg Enery Selewi (katikati|)akifatilia mchakato mzima wa kumsaka mlimbwende wa mkoa.
Niwashiriki wa Miss Kagera wakipita jukwaani kwa mavazi mbalimbali kama ya ufukweni na vazi la ubunifu.Mshindano haya ya vodacom Miss Kagera yalifanyika jana kwenye ukumbi wa linas Night club.Na yameandaliwa na Angers Entertaiment chini ya mkurugenzi wake Mr Josephat Rwebangira.
Next Post Previous Post
Bukobawadau