Maadhimisho ya Siku ya U shirika Duniani Kitaifa yamefanyika Leo 28.6.2011 Mkoani K agera.
Vijana na Wanawakenchiniwameshauriwa kujiunga kikamilifu katika vyama vya Ushirika ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mwandisi Chiristopha Chiza katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Ushirika duniani ambpo kitaifa imefanyika mkoani Kagera.
Naibu Waziri Chiza amesema kuwa iwapo vijana wote watajiunga katika vyama vya Ushirika na kuacha tabia ya kutegemea ajira za Serikali ni dhaili kuwa nchi itakuwa na maendeleo.Pia Mwandishi Chiza ameeleza kuwa Maadhimisho haya yaliofanyika kitaifa Mkoani Kagera kwenye viwanja vya Jimkhana manispaa ya Bukoba ni ya kumi kufanyika nchini na niya 89 Duniani.
Banda la Chama cha Ushirika Wilaya ya Karagwe KDCU LTD.
Mzee ambaye mpaka ivi sasa anatumia mashine yake ya kusaga kahawa inayo onekana katika bicha.Ni sehemu ya kivutio katika maonyesho.
Mwandishi Christopha Chiza akiwahutubia wananchi wa M koa wa Kagera waliohudhulia katika siku ya Ushirika duniani illiofanyika katika viwanja vya Jimkhana manispaa ya Bukoba.
Banda la Tanica katika maonyesho ya Ushirika.