Bukobawadau

UFUNGUZI WA SALEWI CUP :Waanza kwa Kishindo Uwanja wa Kaitaba!!!

Wananchi MkoaniKagera wametakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuendeleza kauli mbiu ya ulinzi shirikishi.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa polisi Mkoani Kagera bwana Henry Salewi katika ufunguzi wa Ligi ya Salewi Cup inayozikutanisha timu kumi na sita kutoka katika Manispaa ya Bukoba.

Kamanda Salewi amesema kuwa jeshi la Polisi limeweka mfumo wa Polisi kata ili kuwawezesha wananchi kuwa karibu na Jeshi hilo. Pia Kamanda Salewei amewataka vijana kuachana na Ualifu na kujikita katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera akizungumza na Wachezaji pamoja na Wadau wa Michezo katika ufunguzi wa Kombe la Salewi. Michuano hiyo imeanza leo katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Ambapo timu ya Kashai imeibuka Kidedea kwa kuifunga
timu ya Kitendaguro kwa mabao 3-0

Afisa Tawala wa Wilaya ya Bukoba Mjini Bwana Gidion Ndyamukama ambae ndie mgeni Rasmi akifungua Salewi Cup.
Shughuli za ufunguzi zilianza na maandamano ya Jeshi la Polisi
Baadhi ya wadau wa mpira nao awakuwa nyuma katika kushuhudia kile kilichokuwa kinaendelea.Anaonekana Ndg Msese na Ndg Ernest Nyambo wakijisogeza Jukwaani.

Waamuzi wa Mpira wakiwa tayari kusalimiana na Mgeni Rasmi.
Kikosi cha Timu ya Kashai.
Pichani anaonekana Mgeni Rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Tumi ya Kitendaguro.Tayari kwa Mpambano ambapo timu ya Kashai imeibuka kidedea kwa kuifunga Kitendaguro jumla ya mabao 3-0 kama anavyo tujulisha Mwanahabari wetu.By Mc
Next Post Previous Post
Bukobawadau