Bukobawadau

MAMISSS KATIKA TOUR CHINI YA KIROYERA TOURS NA SMART HOTEL.

Msimamizi wa shamba la kahawa akijaribu kuwaelekeza mamiss wetu juu ya kilimo cha kahawa na faida zake,Shamba hili lipo chini ya Kiroyera tours ambao niwadhamini wakubwa wa Miss Kagera 2011.
Mamiss wakiwa kwenye Pango la kyamnene sambamba na wadau wengine kutoka kushoto ni Dj Sley na wa pili kutoka kulia ni Emanuel Ernest Mbaule(doctor)wote wa 88.5 kasibante FM Radio ambao pia niwadhamini wa miss kagera 2011.
Wadau katika picha ni mratibu wa shughuli nzima ya Miss Kagera na Mkurugenzi wa Angels Entertaiment kutoka kushoto ni Mr Joseph Rwebangira na wa pili ni Mr Abdulmarick Tungaraza(Dj Max).

Angels Entertaiment kama tunavyo elewa ni mabingwa wa kuandaa matamasha mbalimbali kama ilivyo kuwa mwaka 2009 Miss Dar City Center na kuwapata warembo watatu bora walio ibuka Wwashindi miss Tanzania,nA mwaka jana 2010 ndio waandaaji wa Miss Mwanza na 2011 wamevuka sasa wapo mkoani Kagera.

Anaonekana Mr Hadam (Dj Wabago) kwenye mapolomoko ya Msitu wa Kyamnene Maruku.
Ni Mr Joseph(Jose)wa Angels Entertaiment na Dj Slay wa 88.5 Kasibante Fm Radio.
Hivi ndivyo camera yetu ya wadau ilivyo shuhudia tour ya Mamiss sehemu za vivutio mbalimbaliza siku 2 kabla ya mpambano wa kumsaka Mlimbwende wa Kagera 2011.Mashindano ya kumsaka Miss Kagera yatafanyika kesho kutwa tarehe 24.6.2011 katika ukumbi wa Linas Night club..na kusindikizwa na Msanii bora nchini mwenye tuzo tano 20%.

Shughuli hiyo itashereheshwa na Bebari la Kihaya Mr Mjuni Silvesta maarufu kama Mpoki wa Orginal Comedy.Hii siyakukosa ndg Wadau.
Next Post Previous Post
Bukobawadau